Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Voda ni wezi sana nyie... Yaani unit zipo 125 lakini mnaniambia kuwa zipo 50..

ACHENI WIZI
 
Vodacom. your services around Kibaha are very erratic. have you sunk that low. Please confirm you have received this and you are working on it.
 
Nyie voda mitambo yenu mnayo funga maeneo ya mpakani ni mibovu au??? Maana unakuta mitambo yenu ipo mipakani na ukiwa na cmu hapo inasoma mitandao ya nchi nyingine
 
Huduma zenu za m pesa zina harufu ya wizi unatuma pesa baada ya hapo sms inayorudi ya muamala haionyeshi gharama ulizokatwa kwa huduma hiyo ukiangalia salio unakuta umekatwa pesa nyingi huo ni wizi hebu rekebisheni hilo tigo kwenye hili wao wako vizuri sana
 
Kwa ujumla hao jamaa lazima huwa wanashirikiana TCRA haiwezekani chombo kinachosimamia walaji kikawa kimya. Kwa maoni yangu tuiunge mkono TTCL maana ni shirika la serikali hata kama tukadhulumiwa ni kama pesa ilitoka mfuko wa kulia kwenda kushoto.
 
Mmebadilisha menu,toka juzi najaribu kuwapigia ili niongee na huduma kwa wateja,lakini inashindika kuunganishwa, tatizo ninini au mmeamua msiwe mnaongea na wateja?

Matatizo ambayo yanahitaji maongezi ya moja kwa moja kati ya mteja na wahudumu mmeona hayana maana au?
 
NILINUNUA KIFURUSHI CHA CONTINENTAL DECORDER KWA M-PESA TOKA 03 OKTOBA 2018 KWANINI HAMJATUMA HIYO HELA KWA CONTINENTAL?

USHAHIDI WA FEFHA NILOTUMA NI HII SMS YENU:

5J321PDPA0S 03-10-2018 10:21:38 Pay Bill to 333355 - CONTINENTAL DIGITAL Acc. 8123403687351180 333355 - CONTINENTAL DIGITAL Completed TZS Tsh-11,999.00

Acheni ubabaishaji bwana pelekeni hiyo fedha CONTINENTAL au irudisheni kwangu....
.
 
wadau naombeni msaada jinsi ya kununua bando kwenye modem ya vodacom nimejaribu kuweka *149*01# pale vodacom service kwenye kipengere cha activate bundle lakini natumiwa SMS kuwa alama niliyotumia siyo sahihi
 
kifurushi cha usiku mmeandika masaa 24 badala ya masita kwani ni tokea saa tano hadi kumi na moja jaribuni kurekebisha
 
Kwa ujumla hao jamaa lazima huwa wanashirikiana TCRA haiwezekani chombo kinachosimamia walaji kikawa kimya. Kwa maoni yangu tuiunge mkono TTCL maana ni shirika la serikali hata kama tukadhulumiwa ni kama pesa ilitoka mfuko wa kulia kwenda kushoto.
ni bora aisee kuliko kuwapa hawa matapeli me wananikera kinoma serikal imetulia tu tcra ndo hawana hta mpango
 

Nilifikiri ni mimi tu, nishawachoka hawa jamaa, niliweka salio lazima wakate, ukiwapigia wanakwambia eti ulijiunga na huduma fulani wakati si kweli, wananielekeza kuitoa, nikiwema tena inakuwa hivo hivo.

Dah mpaka nimeamua kuwacha wakate tu
 
Mimi ni mwanahisa wa kampuni yenu na hivi karibuni mmetangaza kuwa mmetoa gawio. Swali langu ni muda gani unapita baada ya kutangaza wanahisa wanapata gawio? Swali la pili je vodacom wana dividend policy?
 

Kiukweli mnaboa Sana hasa kuiba muda wa maongezi unaobakia kwenye Simu, yaani ukibakiza hata shilingi 100 baadae ukiangalia huikuti yaani mpaka inalazimu kuwa unajiunga vifurushi vyenu bila kupenda, Kiukweli huo wizi sio mzuri ila za mwizi 40, ipo Siku tutashtaki na hapo mtaona watanzania watakavyo funguka msifikiri hatuoni mnavyotuibia.

Kingine Sms zenu za matangazo imekuwa nyingi mpaka kero yaani kwa siku mtu unapata sms zaidi ya 50 mi sipendi Mara Tatumzuka, Bico, Sportpesa, Dakapesa, Mojabet, Bado bado zakwenu Kiukweli imekuwa kero Sana, sasa uwe na mitandao miwili hapo ndiyo zinatawala zenyewe tu mxiuuuuuueeei
 
Hata mimi mkuu kama tumefanana maana nlisafir kama miez miwil nikasahau sim moja ya voda hom kurud nikakuta dogo kaitia jino haisomi nikaenda voda na lain mkononi wakanambia namba tano nikataja wananiambia hazikubal mwishoe et nisajil nyingine na akat ile nlikuwa naitegemea kupigiwa tena wengi namba zao nlikuwa sina wao ndio walisev zangu namba 0744470135 .ilivyoshindikana nikamaind had leo situmiag voda
 
Samahani. Nataka kujua taarifa zangu za hisa. Sikuhudhuria mkutano wa wanakosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…