Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Ninakerwa na message nyingi nazopata baada ya kununua bundle zangu via MPESA. Ukinunua bundle tu message si chini ya 6, kuna ya M-PESA, MPESA, VODACOM, TUZO POINT blah blah...... tafadhali sana itafutwe njia mbadala sio fair kutushambulia inbox na message zote hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini mnacharge Ussd code kama za NMB, NBC, CRDB, AZAM NK? , isipokuwa zinazotumika kwenye mitandao wenu, mbona hizo code wenzenu Hawa charge kama tigo na airtel?

Sent from my Infinix-X551 using Tapatalk
 
Okey Here it It. Mwaka jana Vodacom waliniunganisha na huduma yao ya Game Lounge ambayo wala sikuwahi kujiunga nilipolalamika kwenye Twitter account yao wakasema kwamba nijitue, kumbuka kwamba kujitoa unalipia, nikajiuliza how comes kwamba waniunge wao bila mimi kutaka alafu kujitoa nijitoe mimi kwa hela? kujituoa ni TZS 150/= hii ni pesa ndogo kwa kuiangalia ila ni ujinga wa hali ya juu kuingia Gharama ambayo haina msingi.

MWAKA JANA:
Wakanitumia ujumbe kwamba huduma ya Game Imewekwa upya!. Nikaisoma sms nikatulia maana najua kujitoa ni hela.

Siku ya jumapili tarehe 3/02/2019 wakanitumia sms kwamba nimekatwa TZS kwa kujiunga kwenye Gemlounge ambayo sijawahi kujiunga. Sasa hapa Voda wameshasepa na TZS 500/=.

HAPA KUNA WIZI!. Kwenye tangazo la kwanza wanasema watakata tzs 50/= kwa wiki lakini kwenye sms ya makato naona hela iliyokatwa ni TZS 500/=.

This is unethical and unprofessional, Return my money.





LEO TENA wamelamba 150 Kwa ajili ya Hilohilo Game.


VODACOM TANZANIA nahitaji Pesa zangu zirudi Haraka sina mchezo wa kujiunga na huduma ambazo situmii.
 
kuna mtu amenunua till ya mpesa kwa mtu na baadae imezingua na kuonyesha emmegence muda wote na hana detail za hyo lain ..pia kuna hela sijui mnaweza kumsaidia je ?
 
Hawa viumbe hawafai hata kidogo mimi nishatupa line kitaambo....ukiweka mb500 ukiingia jf tu nusu saa imekwisha,nipo airtel natanua hao voda wapuuzi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
VODACOM M - PESA.
Hivi ni vigezo gani ninastahili ili kuanzisha Vodashop?
Naomba mnijibie hapa sio mnidirect Vodashop tena.


Nahitaji sana kufikia lengo hili.
 
hureeeeeèeeeee nice one,wakiendelea kuzingua
tunahamia TTCL rudi nyumbani kumenoga.
 
vodacom Tanzania naomba kufahamishwa,hii offer ya DAR SUPA UNI Tsh2,500/= per week imesitishwa ktk line yangu au vipi maana siipati!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
vodacom Tanzania naomba kufahamishwa,hii offer ya DAR SUPA UNI Tsh2,500/= per week imesitishwa ktk line yangu au vipi maana siipati!View attachment 1022357

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
mkuu hata mimi nangojea wakujibu, kwasasa nimeiweka pembeni laini yao maana sasa huu ni upuuzi! wasiporudisha basi nahamia mtandao mwingine mazima uzuri ninazo laini za mitandao yote.
 
habari mimi nina shida na meseji niliyotuma 2018 tar 6 mwezi wa 10 siku ya jmos mida kama ya saa8 mchana nikiwa maeneo ya chang'ombe kwenda kwa General Manager wa kampuni fulani ya kutengeneza rangi iliyopo maeneo ya maduka mawili chang'ombe kama ushahidi wa kesi mahakamani
mimi nimeipoteza kwenye jumbe zilizotumwa( sent message)
nifanyeje ili nipate hiyo jumbe
 
Voda com ni wezi mno tena mno,leo nimejiunga mb500 nimeingia jamii forum ndani ya dk 6 wananiambia bando langu limekata nilikasirika mno .hivi mnachukulia pesa tunaokota sio??na sio mara ya kwanza kunifanyia huu uhuni...nimewachoka kesho nahamia airtel kwenye afadhali.
pumbavu sana
 
halafu hampo serious na kazi yenu, totally inaonesha nyinyi ni wababaishaji mara ya mwisho kuingia humu ilikuwa mwaka jana last seen ni 3 dec 2018..mnatatuaje malalamiko ya watu humu?? kulikuwa kuna umuhimu gani wa kuanzisha thread ya malalamiko na maswali??
mitandao ya bongo upigaji tu πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜•πŸ˜•πŸ˜•
 

MNAZINGUA
 
Leo vodacom mnashida gani ukipiga simu zinakata tu ukiweka salio haliingi ukiangalia salio hamna tatizo ni nini tupeni hata taarifa basi siyo kuja kuomba samahani baadaye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Voda kunatatizo gani arusha?.Hatuwezi kuongeza salio, kujiunga na vifurushi wala kuangalia Salio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…