Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Sera ya TTCL ingebadilishwa ili iendane na wakati tulionao hivi sasa wa kibiashara ya mawasiliano SIM nchini sera hiyo inyotumika hivi ni toka shirika ninanzishwa miaka hiyo likiwa halina mshindani kumtegemea mh Rais awapigie Debe bila kutangaza huduma zenu kwa watumiaji wa sim nchini itakuwa ngum kwenu kupambana wapinzani wenu sokoni mitandao ya SIM inajitangaza Sana kuhusu huduma zao nyinyi nyinyi uongozi WA ttcl mnamtegemea mh rais na mshatoa gawio matangazo badiliken na sera badilisheni indane na wakati tulionao sasa
 
HARUFU YA UTAPELI/UDANGANYIFU WA VODACOM NA M-KOBA YAO

Habari wakuu!

Kuna nini nyuma ya pazia kwenye hii M-Koba ya Vodacom? Naitafsiri kama wizi/utapeli/udanganyifu, inaonekana ni njia wanayoitumia kukusanya hela za watu pengine na kuzifanyia biashara ama kazi zingine za kiuchumi.

Haiwezekani kwenye akaunti kuna hela lakini kuitoa haitoki licha ya kufuata taratibu zote za kutoa pesa (Katibu kuanzisha muamala, wajumbe wawili kuidhinisha, Mhazini kuidhinisha na mwisho mwenyekiti kuidhinisha). Lakini hakuna hela inayohama. Na kwa sasa ni mara ya tatu sasa bila mafanikio, nikiwauliza wanasema hela haikwenda jaribu tena.

Kingine, wanasema kuhamisha pesa kutoka hiyo Akaunti ya M-Koba kwenda kwa mwanachama ni bure lakini tulifanikiwa kufanya muamala wa kwanza na ndio ukawa wa mwisho hadi sasa, ujumbe wa salio ulioletwa ukawa tofauti na salio tulilolitarajia maana ilipungua 10,000. Baada ya kuwauliza wanasema ujumbe umekuja kimakosa lakini salio halijapungua kwenye lile tulilolitarajia (kilichonistua ni kwamba mfumo wao haujui hesabu? Maana ujumbe wa kuhamishwa pesa ulienda kwa wajumbe wote na kias cha salio lililobaki kwenye akaunti).

Ku-deposit hela kwenyewe hakuna shida, hela zinaingia vizuri mno kutoka M-pesa kwenda hiyo M-Koba. Kuitoa sasa ndio udanganyifu unapoanzia. Wanasubili hadi waifanyie biashara kwanza ndio watoe?

Anayeweza kuwa-tag tafadhali.
 
@Vodacom Tanzania
 
Acha kuchongea watu wafukuzwe kazi, kama anamapungufu ongea nae umweleze
wanazingua hawa wahudumu wa voda shop kuna mmoja nami nitamtaja humu ananizingua kunipa line yangu ya M-PESA eti kisa sijampatia elfu kumi ya kuiactivate hiyo line
 
Katika watu wasiojielewa basi ni nyinyi hasa hilo duka lenu la victoria,muna nyodo na njaa.......

Yaani munataka mteja awabembeleze nyinyi aiseeeehhhh

Nimeenda kusajili line kwa alama za vidole bahati mbaya mwanzo nilisajili na kitambulisho cha kupiga kura na kwasababu picha zinaonekana tofauti kwa mbali kutokana hii nimepiga miezi miwili iliyopita na nyingine nilipiga miaka mitano iliyopita eti wanadai affidavit.....hawawezi kunisajiri hahahahah

Wakati tigo,airtel na halotel wamenisajiri bila vikwazo.......


Aiseeeeh hiyo imekula kwenu
 
Kama huu ukurasa bado Voda mnapitaga napenda kuwajulisha kuwa kuna hujuma inafanyika ofisini kwenyu kwa mtu/watu walio zamu kuanzia saa kumi kamili hadi saa kumi na moja na dakika ishiri leo hii 2/11/2019.

Sitasema hapa ni ni lakini hii ni hatua ya kwanza ikiwa ni taarifa itakayofanyiwa kazi
 
Habari mm nina tatizo kwenye network inaonyesha mtandao upo lakini nikiingia tu mtandao unakata sijui tatizo nn
 
voda punguzeni kututumia SMS ambazo hazina ulazima zinakera... kila cku mnarudia SMS zilezile alafu zinaingia nyingi dah!
 
mna gharama kubwa sana kila siku bei za vifurush na makato ya mpesa yanazd kua makubwa...kwa cc tusiokua na kaz mnatuumiza
 
Katika kifurushi cha Kaskazini Offer kuna chaguo la dk 150 voda-voda, dk 15 mitandao yote na mb 1024 kwa siku tatu, kwa shs 1,500/=. Leo ni mara ya tatu nanunua kifurushi hiki lakini ukiangalia salio baada ya muda mfupi tu unaambiwa una dk 0 mitandao yote ambapo nakuwa bado sijapiga simu yoyote.

Ina maana kwamba kwa siku tatu hizi nimeuziwa kifurushi hewa cha dk 45 mitandao yote, licha ya kwamba leo nimepewa ofa ya dk 15 voda-voda lakini nilipouliza salio nikaambiwa nina dk 10 voda-voda! Kama ndivyo mnavyowafanyia wateja wote basi bila shaka mnatuibia pesa nyingi sana. Sikupenda kutumia lugha hii, ila sioni kama hii inatokea kwa bahati mbaya.

Naomba mtoe maelezo ya kutosheleza juu ya huu udanganyifu ili kurejesha imani yetu kwenu kwamba hamkuwa na nia mbaya nyuma ya pazia, na tutendeeni haki kadri mnavyoelekeza kwenye menu zenu za mauzo.
 

Toka muda wa saa moja asubuhi mganza kagera mawasiliano hakuna tatizo litakua ni nini?
 
Kwanini tunapopiga 100 tunasikiliza mambo mengi yasiyotuhusu mfano mtu unataka kuongea na wahudumu utapita michakato miingi ingekuwa vizuri tuweze kuongea na wahudumu kwa urahisi
 
Nataman sana lifanyiwe kazi tuweze enjoy katika nyanja mbalimbal za mawasiliano
 
Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano Tanzania,ifuatilie kwa makini muda na ubinyaji wa vifurushi unaofanywa na mitandao ya mawasiliano nchini kama vile Vodacom ,kumekua na ubinyaji wa makusudi wa muda na kasi ya bando za internet

imetokea mara nyingi unanunua kifurushi cha bando la internet mfano 1 GB na kuendelea wanachofanya wanafanya data limit na muda unazidi kwenda hata ukiingia katika kuitumia inakuletea 0.0/KBS kwa muda mrefu sana huwezi kutafuta au kupakua unachostahili katika mtandao husika, hiyo ni aina fulani ya kuwaibia wananchi watumiaji wa vifurushi husika,hivyo mamlaka ya mawasiliano Tanzania fuatilieni hilo maana haina maana ya kusema wanyonge wakati mitandao inawanyonya wananchi.
 
Achana nao njoo Halotel ule bata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…