Tetesi: Vodacom Tanzania wasitisha utoaji wa Line mpya za Uwakala za M-Pesa

muta ngegi

Senior Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
167
Reaction score
129
Habari za muda huu wanaJF!

Bila kupoteza muda kuna tetesi kuwa Vodacom hawasajili tena laini mpya za uwakala wa M-Pesa.

Mwenye taarifa tafadhali atueleze nini kimetokea huko.
 
Itakuwa wanafanya maboresho au idadi ya wateja wa mobile money wamepungua sana.
 
Ni kweli nilizungumza nao siku si nyingi. Wakasema wamesitisha huduma hiyo kwa sasa. Wakanijibu pia pindi wakiirudisha watatoa taarifa kwa umma.
 
Hili suala lilikuwepo tangu mwezi wa sita, kabla hata ya kutangazwa kwa TOZO. Binafsi wakati nasajili line ya uwakala, wakala mkuu wa lile eneo alinidokezea jambo hilo.

Ya kwamba ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni, wangesitisha zoezi la kusajili mawakala wapya.
 
Labda hakusema shida nini mkuu?
 
Labda hakusema shida nini mkuu?
Inawezekana labda wanataka kubadili mfumo wa maombi ya uwakala. Ila binafsi naamini hii ishu haina mahusiano na kupanda kwa tozo!

Ingawa ni ukweli usio na shaka, biashara ya miamala imeyumba katika baadhi ya maeneo, tangu zilipo ongezwa tozo. Kama sisi mawakala wapya, ndiyo tunaisoma namba kweli kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…