Vodacom Tanzania yafanya Uboreshaji mkubwa wa Mtandao ili kuhakikisha mustakabali imara na wa muunganiko zaidi

Vodacom Tanzania yafanya Uboreshaji mkubwa wa Mtandao ili kuhakikisha mustakabali imara na wa muunganiko zaidi

Vodacom Tanzania

Official Account
Joined
Aug 12, 2013
Posts
324
Reaction score
126
Ndugu Mteja,

Tunapitia kipindi cha maboresho muhimu kwenye mifumo yetu ya TEHAMA kwa lengo la kuboresha zaidi huduma. Katika siku chache zilizopita, huenda umekumbana na changamoto katika matumizi ya huduma zetu.

Maboresho haya makubwa ya miundombinu yetu ya TEHAMA yanalenga kukuletea huduma bora na ya uhakika zaidi. Wataalamu wetu wanajitahidi kuhakikisha kuwa huduma zako zinaendelea bila kuathirika kwa kiasi kikubwa tunapotekeleza maboresho haya muhimu. Tunatarajia kukamilisha maboresho haya ifikapo katikati ya Novemba, na baada ya hapo, mtandao wetu utakuwa imara zaidi kwa manufaa yako na wateja wote.

Tunakushukuru kwa uvumilivu na uelewa wako wakati huu. Maboresho haya ni kwa ajili ya kukupelekea huduma bora zaidi sasa na kwa siku zijazo.

Asante kwa kuendelea kuwa nasi.

Uongozi wa Vodacom Tanzania
29 Oktoba 2024​

FOR ENGLISH AUDIENCE

Dear Customer,

We are currently working on important upgrades to our IT systems to enhance your Vodacom experience. Over the last few days, you may have experienced some disruptions in our services.

These interruptions are due to ongoing major upgrades to our IT infrastructure, which are designed to enhance the quality and reliability of your Vodacom experience. Our teams are working diligently to minimize any impact on your service as we make these significant improvements. This exercise is planned to conclude by mid November, after which we expect a stronger, more resillient network to benefit all our customers.

We sincerely appreciate your patience and understanding during this period and want to reassure you that these upgrades are essential to serve you better, both now and in the future.

Thank you for your continued trust in Vodacom.

Vodacom Tanzania PLC
29th October, 2024​

Voda Eng.jpg
Voda Kisw.jpg
 
Bei za Voda zipo juu sana yaana tunaishi na makaburu! ukitoa hela kwa wakala kwaa voda au hata lipa nambaa ni bei juu kuliko wenginee!

Nikiwa nalipa kwa line ya tigo kwenda voda ni bei juu kuliko wengine!

Nimeamua line yangu ya voda kuiweka pembeni kwanza mpaka bei zishuke
 
Taarifa kwa wakati ndio kuendana na kasi ya wateja. Mko vizuri.
Ila hamjaspecify ni nini ambacho kitaathilika au chochote kikitugomea tunajiongeza?
 
Maboresho mwezi mzima au JANJA JANJA mnaleta?

Hivi hii nchi ina wataalamu kweli au naota? MWEZI MZIMA?

Yaani kukorokochoa hivyo vikompyuta ndio mwezi mzima?

Ole wenu miamala yangu igome, yaaniii nimejipanga kabisa kuwafikisha MAHAKAMA KUU mnilipe fidia ya BILIONI SABA NUKTA SITA ZIRO.

Sitanii. Nimechokaaaaahhh, au nitawafuata huko ofisini kwenu niwacharaze bakora kabisa.

Kwanza mnatuibia sana nyie MPESA ZETU na BANDO ZETU. MAJIZI WAKUBWA.

Cc: Mbaga Jr ledada Kalpana Kapeace Bantu Lady binti kiziwi mshamba_hachekwi Extrovert Lamomy Poor Brain dronedrake
 
Sio yafanya, hii kauli inaonesha mmekamilisha mlichokuwa mnakifanya, toeni kauli kwamba "Mmefanya na mnaendelea kufanya" Msituchanganye!
 
Da! Mnatusesa sana. Shida hawa wengine internet ni kichefuchefu, tulikuwa tunaona angalau nyinyi
 
Na hata kama mnajinasibu kuwa mnaboresha ila sidhani kama kuna chochote kitakachobadilika
 
Mnatuibia BANDO ZETU lakini mtandao duni.......kazi kutafuna hela zetu tu.

Hizo hela mnazotuibia kwanini msizitumie kuimarisha mtandao? au zote mnazimeza tumboni kama MAFISI?

Halafu vile vimeseji vyenu uchwara vya kunikata shilingi mia kwa siku MKOME na MSHINDWE.

Mkinikata hata senti moja bila ridhaa yangu ndio MTANITAMBUA!
 
Ndugu Mteja,

Tunapitia kipindi cha maboresho muhimu kwenye mifumo yetu ya TEHAMA kwa lengo la kuboresha zaidi huduma. Katika siku chache zilizopita, huenda umekumbana na changamoto katika matumizi ya huduma zetu.

Maboresho haya makubwa ya miundombinu yetu ya TEHAMA yanalenga kukuletea huduma bora na ya uhakika zaidi. Wataalamu wetu wanajitahidi kuhakikisha kuwa huduma zako zinaendelea bila kuathirika kwa kiasi kikubwa tunapotekeleza maboresho haya muhimu. Tunatarajia kukamilisha maboresho haya ifikapo katikati ya Novemba, na baada ya hapo, mtandao wetu utakuwa imara zaidi kwa manufaa yako na wateja wote.

Tunakushukuru kwa uvumilivu na uelewa wako wakati huu. Maboresho haya ni kwa ajili ya kukupelekea huduma bora zaidi sasa na kwa siku zijazo.

Asante kwa kuendelea kuwa nasi.

Uongozi wa Vodacom Tanzania
29 Oktoba 2024​

FOR ENGLISH AUDIENCE

Dear Customer,

We are currently working on important upgrades to our IT systems to enhance your Vodacom experience. Over the last few days, you may have experienced some disruptions in our services.

These interruptions are due to ongoing major upgrades to our IT infrastructure, which are designed to enhance the quality and reliability of your Vodacom experience. Our teams are working diligently to minimize any impact on your service as we make these significant improvements. This exercise is planned to conclude by mid November, after which we expect a stronger, more resillient network to benefit all our customers.

We sincerely appreciate your patience and understanding during this period and want to reassure you that these upgrades are essential to serve you better, both now and in the future.

Thank you for your continued trust in Vodacom.

Vodacom Tanzania PLC
29th October, 2024​

View attachment 3138323 View attachment 3138324
Mnauza taarifa za wateja wenu, wanatekwa na kuuawa, halafu hata hamjali
 
Back
Top Bottom