VODACOM vifurushi vyenu vya kimataifa vinashangaza sana!

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Sitatumia maneno mengi katika hili. Wanasema picha zinazungumza maneno 1000.

Ya kwanza ni hapo Rwanda tu unapoweza kwenda hata na basi.



Ya pili hapo chini ni huko Marekani, Ulaya na hadi China ambako hata Bombadier hazifiki.



Embu tupeni maelezo.

PS. Kuna mrembo wa kinyarwanda nataka kumcheki ila vifurushi vyenu vinanitisha kidogo. Nahisi nitahitaji kama kilo hivi, hapo salamu tu...
 
Hata mimi ilinishinda eti DKK moja kupiga Kenya 1000 nkaona bora buku utie MBs uongee nae tena live kupitia whatsaap video call.
 
PS. Kuna mrembo wa kinyarwanda nataka kumcheki ila vifurushi vyenu vinanitisha kidogo.
Tumia moja kati ya njia hizi za mawasiliano ni rahisi zaidi kuwasiliana na mtu aliye nje ya nchi.
- Skype (video /audio)
- Zoom (video/ audio)
- Whatsapp (Video/ Audio)

Hapo ukiwa na UNI bundle ya 2,000 unatumia kwa siku kadhaa.
 
kwa kifupi ukipiga simu njee ya nchi. kule inakofika kuna gharama mtandao wako unalipia kulingana na muda uliotumia kuongea. So Rate ya kupiga njee inategemea vitu vingi but main factor ni termination charges za call kwa mtandao husika ama sometimes nchi husika kama serikali inaregulate hizo charges.
 
Sasa kelele zote hizi za wanasiasa kila siku kuhusu mahusiano ya Afrika Mashariki ya nini kama jambo kama hili halijaonekana muhimu? Hivi ndiyo vitu vinaweza kutuweka karibu kwanza kabla mambo ya siasa hayajaingia. Yaani tuna hadi Bunge la Afrika Mashariki halafu gharama za simu kati ya nchi na nchi ziko hivi? Kuna jambo haliko sawa.

Wengine tunawaza kwenda kutafuta mke huko!!

Whatsapp calls siyo nzuri siku hizi kwenye simu yangu sijui tatizo nini. Na huyu mrembo na yeye ana tatizo hilo hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…