Ulukolokwitanga
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 8,397
- 7,974
Huku maeneo ya Southern Highland minara mingi ya Vodacom (Kama sio yote) inaungurumisha majenereta kila siku. Toka nimerudi home kuhesabiwa yapata wiki moja sasa kila mnara wa voda unatumia jenereta. Nikaamua kumuuliza jamaa yangu ambaye ni mdau wa mawasiliano kulikoni kaniambia kuwa Voda wanadaiwa bili kubwa hivyo wamekatiwa umeme na Tanesco, mdau mwingine akasema kuna bifu kati ya Voda na Tanesco ambayo ina mizizi katika malipo ya Dowans hivyo Tanesco wamewakatia umeme voda kuwakomoa. Mdau wa mawasiliano kaniambia kwa wastani mnara mmoja bili yake kwa mwezi ya umeme haizidi laki tano, ila ukiungurumisha generator mwezi mzima gharama inazidi milioni tano. Pia inaliingiza taifa katika matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za kigeni kununulia mafuta ya ziada ku-run minara.
Kama kuna kdau yeyote humu jukwaani anajua ukweli atujuze ili tulijadili hilo bifu kwani kama lipo madhara yake kiuchumi ni unprecedented. Hali halisi ni kuwa karibu minara yote ya Voda Iringa na Mbeya inaunguruma kwa majenereta, sijui huko kwako...