Vodacom wamevujisha taarifa zangu(?) - Kuweni makini na matumizi yenu ya Simu

Status
Not open for further replies.
yani voda wavujishe taarifa kwa fundi umeme ili wapate gawio la posho ama...!? hahaaahaaaaaa
Mambo mengine yanatakiwa utafakari na siyo ubwatuke tu. Wewe una tatizo walilonalo watanzania wengi. Maneno meengi bila akili. Unajuaje kama huyo ''fundi umeme'' alikuwa aende afanye mengine? Back to topic: hidemyid2019 Ni kweli hizi taasisi zetu za huduma zina watu matapeli wamejipenyeza. Kuanzia benki, kapumpuni za simu na sehemu nyinginezo. Lakini inawezekana vilevile isiwe Vodacom waliovujisha. Inawekana mwenye nyumba wako alipopokea msg katika mazungumzo yake na mtu wa karibu kuna tapeli alikuwa karibu na anakujua wewe akatumia hiyo chance. Au wewe ulikuwa katika mazungumzo yako huko nyumbani kuna tapeli alikusikia na akatumia hiyo chance. Hapa hata Vodacom wakikupeleka mahakamani utashindwa kwani huna ushahidi wa tuhuma zako.
 
mwenye nyumba ni mwanaume, na hakumpa taarifa mtu mwingine yeyote hadi wakati nampigia simu kumwuliza kama ni kweli kamtuma fundi aje
Matapeli ni watu wenye masikio makali sana. Wanajua kupata taarifa kwa njia mbali mbali. Unaweza kuwa uko ndani unaongea na mke wako tena kwa sauti ya chini kabisa lakini wakakusikia. Unaweza kuwa umekaa Bar na rafiki zako mnapiga story na katikati ya story ukasema ''tena nimekumbuka ngoja nimjulishe mwenye nyumba yangu ...... '' na wakakusikia. Kwa kifupi wana njia nyingi mno.
 
Mwenye nyumba ana mke? What if mke/mume ndo kampigia simu fundi?
Mkuu unetumia "Occam's Razor".

Explore the simplest explanation first.

Ila Vodacom kuna kitu kikubwa kinatokea.

1. Rostam kauza hisa zake zote.

2. Kampuni la kimataifa la kutuma miamala kwa sinu "Wave" limejitoa Vodacom kwenda Airtel.
3. Ali Mufuruki anajiuzulu.
4. Watu wanadukuliwa na kususia mtandao.
 
nimejihakikishia kuwa mawasiliano hayo nimefanya mimi na mwenye nyumba wangu tuu, na hakuna mtu mwingine aliyeshirikishwa, sasa inakuwaje yamevuja? kama si mtendakazi ndani yao, basi mifumo yao ni inaruhusu wadukuzi kupata taarifa za mawasiliano ya wateja, kwa kuwa si mara ya kwanza leo, kuna siku nilitoka kuwasiliana na mtu kuwa namtumia pesa, mara ghafla ndani ya kd 5, napokea sms ile hela tuma kwenye namba hii.. kwa kiyo mambo kama haya yanaharibu picha ya kampuni
Nashauri Vodacom wakufungulie mashtaka unawachafua kwa hoja mfu
 
maswali ambayo mimi na mwenye nyumba tumejiuliza kabla sijawapigia simu voda ni haya
1. Huyu mtu amejuaje kuwa kuna tatizo la umeme hapa nyumbani?
2. kama amesikia, je? namba yangu ya simu katoa wapi maana mimi ni mgeni kwenye huu mtaa ninaoishi, hakuna mtu mwenye namba yangu kwenye mtaa huu zaidi ya mwenye nyumba wangu
kwa hivyo bado nina maswali mengi kuhusu hili, na kama si voda waliovujisha mawasiliano haya basi ninaamini mifumo yao imeruhusu waovu kudukua taarifa zetu
 
taarifa zako kuwa unatakiwa ulipe kodi ya nyumba alizipata wapi? ndio maana bado naamini mifumo yetu ya mawasiliano inaudhaifu
 
Swala ,bado unayumia voda hadi Leo? Pole sanaaa
 
wasted sperm
 
Yeah, on an unrelated note though.

I don't think there are any data breaches kutokana na alichosema mtoa mada.
 
Taarifa haina uzito wa kuvujishwa na kampuni lakin inawezekana kuvujishwa na mfanyakazi binafsi kama kumpa mchongo rafiki yake. Tuwe makini sana hali ilipofikia.

Binadamu anakuwa dhaifu sana hata kwa mambo madogo usimuamini 100%

Hapa ndio pakuanzia ili tuweze kuchunguza mawasiliano yetu.
 
Yaan ndugu unaweza ukashtakiwa bila sababu maana umeandika taarifa za kulichafua kampuni bila hata kufikiria kwasababu umemuuliza baba mwenye nyumba kakataa umeconclude na kupost kwa social media hivi....unajua athari anazoweza pata vodacom kwa hii post...How sure ni Vodacom 100% na sio huyo baba mwenye nyumba....TAKE CARE USIKURUPUKE.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…