Vodacom wekeni mambo yenu sawa

waBasila

Senior Member
Joined
Jun 27, 2013
Posts
168
Reaction score
37
Mimi nikati ya mteja wenu wa kudumu na ndivyo nitakavyozidi na siku zote napenda huduma zenu,but takriban ndani ya kipindi cha miezi kama sita mtu unajiunga na cheka ya 1200 au 900 unashangaa unapiga simu moja ndani ya dakika 4 imekata na cheka ushakatwa. NMB mobile unaingia hujafika mwisho inakata na fedha umekatwa,waweza ingia hadi mala 5 ili ufanikishe haja yako,na usifanikiwe kufika mwisho lakini kila unapoingia unakatwa.hii haiendelezi sifa yenu
njema.sijui kama yananikuta mimi tu au wateja wa mkoa wa Arusha tu. yawezekana ni matatizo ya kiufundi sawa lakini jaribuni kupunguza kama ilivyokua mwanzo.nawatakia ufanisi zaidi, kwa maendeleo ya uchumi wa nchi na ufanisi katika kutoa huduma.
 
Nna imani ujumbe wako ushafika mkuu,tena ingekua vizuri kama ungewatumia kwenye tovuti yao, haya jaribu sasa
 
Wizi sasa hivi umezidi kuongezeka katika makampuni yote haya ya simu.
Dawa kutumia benki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…