Vodacom yatangaza faida ya shilingi 170 bilioni

wanzagitalewa

Senior Member
Joined
Jan 25, 2018
Posts
128
Reaction score
84

Mkurugenzi mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao

Kuimarika kwa mapato ya kampuni ya Vodacom kumeiwezesha kupata ya faida ya Sh170.24 bilioni hivyo kuwa na uwezo wa kutoa gawiwo la Sh83.81 kwa kila mwanahisa.

Faida hiyo imepatikana katika mwaka unaoishia Machi 31, 2018 huku maeneo matatu yakibainishwa kuchangia ufanisi huo.

Mkurugenzi mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao amesema maeneo yaliyopata faida hiyo ni katika huduma ambako faida imeongezeka kwa asilimia 5.9 na kufika Sh966.3 bilioni wakati yale ya M-Pesa yakiimarika kwa asilimia 16.7 hadi Sh291.2 bilioni.

Pia, mauzo ya data yakiongezeka kwa asilimia 34.7 na kufikisha Sh141.6 bilioni.

“Mafanikio hayo yametokana na huduma bora tunazozitoa kwa wateja na kuimarika kwa matumizi ya data na mfumo unaoboreshwa kila siku wa fedha mtandaoni.” amesema Ferrao.
 
Na sisi tunaocheza tusua mapene watuangalie maana wanatukamua sana halafu hamna tunachopata kumbe wanaingiza faida pesa ndefu hivi
 
Gawio la sh 83.... which means kama una hisa 10,000 unapata 830,000/= tu..hii ni kwa mwaka right? Kama ulinunua hisa kwa wakati ule hisa moja iliuzwa 850/= which means kwa hisa 10,000 uliwekeza 8,500,000! Anyway pengine sijui mengine yaliyomo but to me its a waste..
 
Wale walioweka hisa kipindi kile watupe mrejesho kama kweli nyumbani kumenoga
 
Na sisi tunaocheza tusua mapene watuangalie maana wanatukamua sana halafu hamna tunachopata kumbe wanaingiza faida pesa ndefu hivi
Bora buku ukanunue mbegu za mchicha upande hata kwenye vifuko, visandarusi, gunia au viroba kama hauna bustani au pa kulimia utavuna ndani ya wiki tatu kuliko kuwekeza kwenye bahati nasibu.
 
H
Hii kununua hisa ni biashara kichaa
 
Watutumie gawio mpesa basi la tsh 10

OvA
 

In fact ukiwasikiliza washauri wa masuala ya uwekezaji wanakwambia ununuaji wa hisa ni 'Risk Business' basically mimi natasfiri kama baishara kichaa.
 
Uzuri wa hisa ni hapa mkipata faida wote mnanufaika
Mkipata hasara wote mnahusika
 
Kumbuka kwamba hisa ni biashara yenye faida na hasara. Ikiwa na hasara shukuru tu kama kampuni haitokufa. Kukiwa na faida tarajia
1. Faida ndogo ya dividend lakini utakua unapata kila mwaka kwa miaka yote utakapokua ukiendelea kumiliki HISA. Na HISA hizo zitakupa gawio kama kampuni ikiridhia
2. Ukiamua kuuza hisa baada ya kua kampuni inatoa GAWIO basi una nafasi ya kupata capital gain.
Kwa hiyo hisa bob zina mapato ya aina mbili ambayo yanaweza kua faida kwako.
1. Divident
2. Capital gain
 
Huwezi kuiita waste wakati hata benki hakuna benki inayotoa interest ya 10% kwenye deposit. Hii inaitwa risk free investment. Usitarajie faida kubwa ila tarajia kutopata faida. Kuna tofauti kati ya kutopata faida na kupata hasara.
Ukinunua bajaji ukampa kijana akuzungushie ili akupe hesabu ya siku unaweza kuirejesha milioni 8.5 baada ya miaka miwili ukikomaa mwenyewe unarejesha ndani ya miezi 12. Ila risk zipo nyingi kuibiwa kuuawa kupata ajali n.k na kujikuta mtaji haurejeshwi tena. Ukisubiria dividend utakaa miaka 10 kwa rate hiyo. Ukisubiria dividend na capital gain pengine unaweza kukaa miaka 3&4 ukarejesha pesa yako na faida juu. Chaguzi ya biashara ni hiyari ya mwekezaji
 
 
Na anasema kwa KILA MWANAHISA sio kila HISA
 
In fact ukiwasikiliza washauri wa masuala ya uwekezaji wanakwambia ununuaji wa hisa ni 'Risk Business' basically mimi natasfiri kama baishara kichaa.
Ununuzi wa hisa wa kusubiri gawio la mwaka ni biashara kichaa, lakini kama ananunua anasubiri bei imeongezeka hata 20 anauza, then anasubiri ishuke ananunua na kuuza ikipanda huyo mtu atapata faida kubwa tu
 

long term! long term long term! biashara ya hisa inahitaji uwe na mipango ya muda mrefu na sio uwaze kuwekeze leo faida uanze kupata kesho! hapana .....unahitaji kuwa na subira

binafsi nina mjomba wangu alinunua hisa kampuni ya sigara tcc kipindi icho kampuni imeyumba

huwezi amini mjomba wangu alishatangulia mbele ya haki lakini hyo hela ya hisa ndyo imesomesha watoto wake mpk chuo kikuu huku yeye akiwa tayari hayupo duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…