Vodafone: Watanzania walio wengi hawapendi mawasiliano yao na viongozi wao kuingiliwa/kurekodiwa

Vodafone: Watanzania walio wengi hawapendi mawasiliano yao na viongozi wao kuingiliwa/kurekodiwa

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
Rais+Kikwete+akiwa+na+Rashid+Othman+Mkurugenzi+Mkuu+wa+Idara+ya+Usalama+wa+Taifa.JPG


Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid

Wakati idadi kubwa ya Watanzania inapinga vikali taasisi za intelijensia kuwafanyia ushushushu viongozi wa siasa na raia wa kawaida, Tanzania inashika nafasi ya pili duniani-nyuma ya Italia-kwa kudaka mawasiliano ya wananchi wake kwa siri.

Asilimia 71 ya Watanzania waliohojiwa katika utafiti uliofanywa na taasisi ya Pew Research Centre ya Marekani walipinga vitendo vya serikali kuingilia mawasiliano ya simu na email ya viongozi wa kisiasa. Asilimia 25 waliafiki vitendo hivyo.

Utafiti huo ulionyesha kuwa Watanzania wanaongoza barani Afrika katika upinzani wao dhidi ya uvamizi wa faragha yao unaofanywa na taasisi za intelijensia.

Hata hivyo vitendo vya kishushushu kufanya ufuatiliaji kwa kuingilia au kunasa mawasiliano vimeshamiri mno nchini Tanzania kiasi kwamba nchi hiyo inashika nafasi ya pili duniani nyuma ya Italia katika vitendo hivyo.

Mwezi uliopita, kampuni ya kimataifa ya simu za mkononi ya Vodafone, ilitoa taarifa inayoonyesha kuwa kampuni yake tanzu ya Vodacom Tanzania ilitoa mawasiliano 98,765 ya wateja wake kwa mashushushu.

Katika ripoti hiyo, Tanzania inatajwa kuwa ni nchi ya pili duniani - katika nchi 29 ambapo Vodafone inatoa huduma - nyuma ya Italia kwa kufuatilia, kuingilia au kunasa mawasiliano ya simu. Italia inashika nafasi ya kwanza kwa mawasiliano 605,601 yaliyoombwa na taasisi za usalama.

Vodafone ilibainisha uwepo wa nyenzo za siri zinazowawezesha mashushushu kusikiliza mawasiliano ya wateja wa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo imevunja ukimya kuhusu vitendo vya serikali kuwafuatilia raia wake kwa ushushushu katika mitandao ya simu na intaneti.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Tanzania, utafiti huo umeonyesha kuwa asilimia 49 ya Wakenya wanaafiki mashushushu kunasa mawasiliano ya simu na email ilhali asilimia 44 hawaafiki.

Utafiti huo unaonyesha kuwa Kenya inaongoza miongoni mwa nchi za Afrika kuhusu ridhaa kwa serikali/mashushushu kuwapeleleza raia.

Chanzo: imetafsiriwa kutoka gazeti la The Citizen (Tanzania)
 
Huu ni ukweli mchungu , mawasiliano,yangu na yako hayako salama hata kidogo....
 
kama ni kwa ajili ya usalama wa taifa , sioni tatizo ili waweze kuwabaini majambazi, magaidi, wahamiaji haramu n.k. mimi nasema Usalama wa Taifa waendelee tu kulilinda taifa.
 
Huu ni ukweli mchungu , mawasiliano,yangu na yako hayako salama hata kidogo....

Kama mnawasiliana kwa mema sidhani kama kuna tatizo na sidhani watakuwa na shida nayo, ila kama mnapanga njama za uharibifu kwa nini wasikudake, lazima udakwe tu.
 
Sioni ubaya katika hili kwa mstakabali wa Taifa.!
 
"You can not promulgate 100% freedom and expect to be 100% safe" Barack Obama
 
Ukiona vinaelea ujue vimeundwa, amani tulionayo ni kwa sababu ya mambo kama hayo. Nimependa sana hiyo, sasa naweza kutembea kifua mbele nikijua kuna full ulinzi.
 
Hii nadhani no sababu mojawapo ya kupungua kwa kiwango kikubwa kwa vitendo vya uhalifu hapa nchini, ona hata magaidi wamnavodhibitiwa tofauti na wenzetu nchi jirani hasa Kenya
 
Hii nadhani no sababu mojawapo ya kupungua kwa kiwango kikubwa kwa vitendo vya uhalifu hapa nchini, ona hata magaidi wamnavodhibitiwa tofauti na wenzetu nchi jirani hasa Kenya

Hiyo ni source ya amani na utulivu tulionao.
 
hawajiamini wanatawala kwa hira lazima wajihadhali wezi wakubwa hao
 
kama ni kwa ajili ya usalama wa taifa , sioni tatizo ili waweze kuwabaini majambazi, magaidi, wahamiaji haramu n.k. mimi nasema Usalama wa Taifa waendelee tu kulilinda taifa.

Usalama wa mafisadi sio wa taifa ndugu
 
Kwani una shida gani kama unafanya mawasiliano yawiyo na madhara katika jamii?
mkuu ukiona hivyo ujue haki sawa ana matatizo, mimi kama nawasiliana na mpenzi wangu, mawasiliano ya biashara n.k nina tatizo gani?
 
Back
Top Bottom