Voices from Within: Kama Moja ya Sababu za Kuitwa Kwake ni Udhalimu, Aliyemfuatia Akifanya Udhalimu, na Yeye Pia ...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi

Angalizo la uchangiaji
Hili ni moja ya mabandiko yangu ya mada za kikubwa,na huwa yanapanda humu mida ya usiku mkubwa wakati watoto wameisha lala!

Hakuna jina la mtu yeyote, limetajwa kwenye bandiko hili. Hivyo naomba sana wachangiaji changieni kikubwa, tusilete utoto humu wa kutaja taja majina, hapa tunakata hoja tuu, kwa hoja kujibiwa kwa hoja na sio hoja kujibiwa kwa viroja, msitaje jina la mtu yeyote humu kwenye mada hii!, Please!.

Leo nilikuwa nasoma bandiko hili humu jf Aibu kwa Mhimili wa Mahakama: Kutoka kutumiwa kama kielelezo cha Utetezi wa Haki hadi kutumiwa kama kielelezo cha kuminya Haki.

Mara nikaisikia ile sauti,the voices from within, ikiniambia kuwa, kama moja ya sababu za kuitwa kwake yule ni udhalimu, uliotokea wakati wa kipindi chake, then na aliyemfuatia akifanya udhalimu, na yeye pia ... (naomba nisimalizie!).

Kama hii the voices from within ni sauti ya kwake YEYE ambaye ni YEYE, then huu ni ujumbe mahsus kwa aliyemfuatia aepuke kufanya udhalimu wa aina yoyote,utakaopelekea na yeye ku ...!

Japo hakuna mwanadamu,wala binadamu yeyote anayezijua sababu za mtu yeyote kuitwa, lakini sote, tunajua fika kuwa everything that happens, happens for a reason!, yaani hata YEYE anapoamua kufanya jambo lolote la mapenzi yake kwa yeyote, analifanya kwa sababu, ila hizo sababu sisi hatuzijui, ni YEYE Pekee anazijua!. Japo hakuna ajuaye sababu za kutwaliwa kaka, isipokuwa Mungu, kuna watu saw it coming, wakasema, wakapuuzwa, akatwaliwa. Dada ukisikia usipuuze hili

Binadamu hatufanani na hatulingani, kuna wenzetu wamejaaliwa jicho la tatu, waliziona hizo sababu, wakatoa ushauri, wakapuuzwa kwa hoja kuwa who are you? , yaani wewe ni nani hadi usikikizwe?!, wakidhani manabii wote lazima wavae majoho na kuhudumu madhabahuni!, hawajui kuwa kumbe kuna manabii majalala Tanzania tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!

Baadhi ya hao manabii majalala wana possess powers za Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo? ambapo
kauli zao ni kauli umba!,wakisema jambo,kama hilo jambo wameambiwa na YEYE , linatokea kweli!"Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia

Naomba kujinasibu humu jf kuwa mimi ni mwalimu wa somo la kitu kinachoitwa karma。Karma ni what goes around,comes around!The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!

Hii karma is real na ipo kweli!,everything happens for a reason!, japo hakuna ajuaye kwanini yule alitwaliwa, lakini there was a reasons,kuna sababu fulani, sisi wa jicho la tatu,tuliziona,tukazisema, tukaziandika, tukapuuzwa, akatwaliwa!。Japo hakuna ajuaye sababu za kutwaliwa kaka, isipokuwa Mungu, kuna watu saw it coming, wakasema, wakapuuzwa, akatwaliwa. Dada ukisikia usipuuze hili

Kwa vile hakuna ajuaye sababu haswa ni nini zilizopelekea yeye kutwaliwa,urais ni kibali ili ufanye mambo kwa namna ya kumpendeza aliyekupa kibali,ukifanya vinginevyo,kibali chako kinafutwa!sababu za kufutwa kibali ni bad karma inaweza kuwa imechangia!。Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Sasa tunapoanza kuona zile sababu za bad karma kama za wakati ule,zinaanza kujirudia wakati huu, hatunyamazi ili kusaidia kuzuia a bad karma isitokee tena!

Kwa upande wangu,mambo yanayosababisha a bad karma kwa Rais wa JMT, ni mambo mawili
1. Vitendo viovu vya kusabasha watu waumie,walie na wavuje machozi,jasho na damu za Watanzania。
2. Ukosekanaji wa haki ndani ya JMT,zikiwemo haki jinai,haki siasa,haki katiba,haki sheria,na haki uchaguzi kwa kutofanya uchaguzi huru na wa haki,bao la mkono na figisu figisu na udhalimu Elections 2015 - Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

Hapa naweka baadhi ya matukio ya bad karma ya awamu iliyopita,nikionyesha nilishauri nini awamu ile,na nimeshauri nini awamu hii。
Enzi ile Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!

Awamu hii Pre GE2025 - Baada ya Mtu Kusema Ukweli Kuhusu Uchaguzi Kuendeshwa kwa Mutatis Mutandis, Tunaomba Uchaguzi Mkuu wa 2025 Uendeshwe kwa Ceteris Peribus!

Kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa, 2024,nikamsisitizia mtu wetu Pre GE2025 - LGE2024 - Ombi Maalum, Kwa Mtu Maalum Achana na Hizi Mutatis Mutandis Kwenye Chaguzi za SM2024 & U/Mkuu2025, Tumia Ceteris Peribus, Utabarikiwa, Tutabarikiwa!

Ushauri huu,ulipuuzwa, tukafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mutatis mutandis zile zile kama za 2019, na sasa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu https://www.jamiiforums.com/threads...r-tufanye-tu-illegal-elections.2346113/,hivyo tunakwenda kufanya tena uchaguzi mkuu wa 2025 kwa mutatis mutandis zile zile za uchaguzi wa 2020!,tukipata matokeo kama ya 2020, pia tuwe tayari kuyapokea na yatokanayo !。

Hitimisho
Haya mabaya yote uanayotokea awamu hii ya hakuna hata limoja Rais analifanya yeye,ni wasaidizi wake,hivyo tumewasisitiza Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma na kwa vile Rais ndie mwenye dhamana, Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe
Tukiweza kuepuka bad karma,tuepuke,tusiipe karma sababu!

Mpaka hapa tulipo,we still have very little time to make it right before its too late, and not only to do the right thing,but also, do it right!。
Where there is a will, there is a way!, kinachohitajika ni kitu kidogo sana kinachoitwa utashi wa kisiasa, a political will!.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Update ya Bandiko hili,
lengo la bandiko hili lilikuwa ni dogo tuu la uwepo wa nia ya dhati ya kisiasa ya kufanya jambo fulani dogo tuu when we still had time. Jambo hilo was just to make it right before it was too late, and not only to make it, by doing the right thing,at the right time and do it right, but very unfortunately, nia hiyo ya kisiasa haikuwepo!, as a result we did a wrong thing, at the right time, but we did it wrong na matokeo yake ndio kama vile, kile kilichotokea, ile October 29 ambao ni udhalimu mkubwa zaidi kuliko udhalimu wowote kuwahi kutokea Tanzania tangu kuasisiwa kwa taifa hili!.

Hivyo sasa, kitu kinachosubiriwa ni kimoja tuu, kama hii sauti ni yake YEYE mwenyewe, then tumsubirie YEYE, Atatenda, ila kabla hajatenda, nimeisikia sauti nyingine ikisema Kufanya Kosa si Kosa, kosa Kurudia Kosa!, Kama Kosa lina consequences, ukirudia, the consequences are the same!. Je Tujiandae for The Consequences au?

Paskali
 
Sijui akili yangu imepungua siku hizi yaani sijaelewa chochote kwa zama hizi za ukweli na uwazi bila kutaka majina ya wahusika wa Uzi naiona hii NI kama Tu ngonjera ni uandishi Tu na utungaji wa maneno hewa.nawaachia wakubwa wenye akili wachangie me napita nilikuwepo
 
Kuna watu mpaka wame Post like Gari lao lakufutwa na punda halafu lina banduki kubwa mgongoni yakutungulia mwewe au kunguru wa znz na wa bara vile vile
 
Naona unatoa milio sana siku hizi..... Kuna dhalimu kama Idd Amin? Mbona Nyerere alikufa akamuacha kama madhalimu hufa mapema? Kagame, Museveni, Mobutu? Ukiwa kiongozi lazima utapitia vibaka wanaotaka kuchezea nchi. Ni halali, ndio maana hata Mungu anasema yeye ni bwana wa majeshi, kazi ya jeshi sio kugawa ice cream...... Pia kasome agano la kale uone wafalme wakipiga misumari kwa maelekezo ya Mwenyezi
 
uzi wa wakubwa huu, watoto hamjalala tu? basi mkalale.
 
Hakuna wa ku make it right, umesema tusitaje watu mimi naomba nimtaje mmoja.

Jana kama sio juzi Prof.Kabudi kasema mwaka huu tunaenda kufanya uchaguzi wa kihistoria, yani hauna makosa wala mawaa kama chaguzi zilizopita.

Maana yake ni kwamba wameridhia hakuna reform yoyote, so no making right of anything.

Jaji Mutungi kavihasa vyama vinavyoshiriki vifanye kampeni za kistaarabu viache matusi na wasiwasikilize wale wasemao hakuba uchaguzi.

Mwenyekiti wa tume huru kasisi tiza uchahuzi upo pale pale.

Huo ni ushahidi there is no making it right of any kind.

Sasa mimi nasema "USIENDE KUPIGA KURA, BAKI NA KURA YAKO NYUMBANI KWAKO".
 
Kalale
 
Unayoyasema ni kweli. Na ningekushauri uache kutumia neno "Karma" maana wewe ni Mkristo hivyo tumia Neno la Biblia kama ifuatavyo:
"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna" Galatia 6:7.
Hili halimhusu tu mtu binafsi bali hata Serikali na vyama. Hivyo tujitahidi kutenda mema.
 
Chakushangaza nikwamba yeye yupo hapo kutokana kifo cha mkubwa wake, jee na yeye hafikirii kwamba kuna kifo?
Unaambiwa muogope mtu asiyemuogopa Mungu.
 
Kwa yanayofanyika, tuna uhakika kuwa utawala uliopo ni wa shetani, kwa sababu unatenda yale yaliyo kiyume na haki na upendo wa kweli, kuiepuka laana ya Mungu, hatustahili kushiriki hata kwa nafasi ndogo kabisa kujishikamanisha nao. La sivyo, nasi tutabeba sehemu ya laana ya huu utawala.

Mwezi October tusishiriki kwa namna yoyote ile kwenye huo ushenzi uliopangwa ili kubariki uovu wanaoufanya.

Siku hiyo ya uchaguzi bandia, watu wajifungie majumbani mwao, wafanye ibada, kuomba ukuu wa Mungu uingilie kati ili utawala wa shetani, unaowamaliza watanzania kwa namna mbalimbali, upate kutoweke nchini mwetu.
 
Yaani huyu naona amechelewesha. Aitwe haraka. Hafai na hafai Leo na kesho. Yaani ni aibu na inasikitisha kwa kile nchi inatendewa kwasasa. Kila sehemu ni rushwa tu. Kila sehemu ukitaka kulipa wanakwambia machine imepata tatizo. No receipt.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…