Voices from Within: Kama Moja ya Sababu za Kuitwa Kwake ni Udhalimu, Aliyemfuatia Akifanya Udhalimu, na Yeye Pia ...

Ukifuatilia matendo ya Hawa wa kuitwa "waaminio Mungu sana" tena hasa kwa kuamini Mungu atatenda baya kwa familia Fulani Ili familia Fulani nyingine ipate raha, utastaajabu mno!!!
Kambona aliombea Nyerere kufa, maalim seif alimuombea Nyerere, cuf wakamuombea mkapa, akina slaa wakamuombea kikwete, akina lema wakamuombea magu, akina lema, lisu wanamuombea Samia, akina heche watamuombea mwengine tena!!!
Ila wao kuingia madarakani hawawezi, ni Mungu tuu awabadilishie viongozi wa CCM na serikali!!!
 
Umesema asitajwe mtu lakin mwisho wa siku unatoa reference na kutaja uongozi uliopita


Ccm tangu lini wanajua kama kuna karma.?? Alafu hizi karma zingeanza tangia awamu ya nyerere mana wao ndio waanzilishi wa dhulma kwa wananchi
 
Hii sauti yako ya within haikupi mambo ya nyetanyahu,trump,drug dealers,majambazi, Khomeini,Alshabab,Wachawi,na wengineo wabaya wabaya,wewe yakwako skuzote inalenga pale pale tu?
 
Umesema asitajwe mtu lakin mwisho wa siku unatoa reference na kutaja uongozi uliopita


Ccm tangu lini wanajua kama kuna karma.?? Alafu hizi karma zingeanza tangia awamu ya nyerere mana wao ndio waanzilishi wa dhulma kwa wananchi
Shida ni Imani ya mtu, ni sawa na wale wanaosali novena, huku wengine hiyo nevena hawaiamini kabsa, unamsalia mtu albadir wakati haamini hiyo kitu, itampataje??!
 
Mtu ambae "hana akili" kamwe hawezi kuchukua ushauri wa mtu mwenye akili..kila neno jema utakalo mwambia,masikioni mwake litakua kama kelele za dharau na dhiaka,Usishangae watu wanao shauri mazuri,wenye mtazamo chanya kwa kesho ya watoto wetu wanateswa na kudhuriwa..

Walisema wazee kabla yetu,sikio la kufa halisikii dawa..
 

This voice from your within is really!

zimetamkwa kauli-umba nyingi sana msimu huu kuliko misimu mingine yote. what said must happen, for the God's sake.

nakumbuka ule usemi wa "sikio la kufa halisikii dawa"

Barikiwa mtumishi. a thread of a week
 
Mpaka hapa tulipo,we still have very little time to make it right before its too late, and not only do right thing,but also do it right!。
Asante kwa bandiko hili,
Muda mfupi uliopita nimesikia maagizo mengine matano anaelekezwa ayafanye kazi ili tuepuke mutatis mutandis na tukimbilie kwa "ceteris peribus ". Lakini mpewa maagizo aliwahi kunukuliwa kuwa anayotabia ya Tembo akinywa Maji kwenye dimbwi la vyura wakiwa na shangwe.

Mtoa maagizo simuelewi aliposimama kama ni salama ama la!!!
 
Mimi nasema na yeye aitwe tu hakuna shida kwani anapita mule mule, hata Baba Mchungaji naye hajataja mtu
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
 
Haya mambo yapo ya Mungu kuingilia Kati Kwa jambo la Dhulma,nilishuhudia mwenyewe jamaa Mmoja mcha Mungu!Mwaka 2013,Watumishi wa kampuni Moja,walimuundia zengwe jamaa ili afukuzwe kazi wakishirikiana na meneja!Wakafanikiwa kweli,jamaa akafukuzwa.Cha kushangaa walikufa mmoja,mmoja na mwingine aliendavkutibiwa hadi India lakini hakupona,mmoja kabla hajafa alitaka aonane na jamaa!Jamaa aliyefukuzwa kazi yupo hadi Leo!.Funzo ni kwamba Mungu hskutaka watambe Kwa kumkomoa jamaa na wao wakicheka.
 
Kama alichofanyiwa Polepole ni udhalimu na umefanywa na watu "wasiojulikana" then watu hao watafutwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake.

Lakini kama ni 'wasiojulikana', then tusiwalaumu, ni watu wa kazi wanaotimiza majukumu yao wako kazini hivyo hawana makosa walikuwa wanatekeleza amri halali, hii maana yake kuna mtu amewatuma!.

This being the case, then namshauri Mtu Wetu, ambaye mimi ni Dada yangu, tena kwa unyenyekevu kabisa, aachane kabisa na watu hawa, watakuja kumponza bure kama walivyomponza yule Kaka yangu, akananihiliwa!.

Nimewaomba sana wasaidizi wake Thread 'Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe' Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe
Hii ni katika kukumbushana tuu, kama ni kweli Humphrey Polepole, ametekwa na wasiojulikana, then hatma yake tuikabidhi kwa aliye JUU kwa sala na maombi.

Lakini kama ni wale wasiojulikana 'wasiojulikana', then tunawaomba kwa kuwashauri, mfanyieni tuu mohojiano kwa njia za kawaida za majojiano, kama akikutikana na hatia mfikisheni kwenye vyombo vya sheria, msiimwage bure damu yake, mtajikuta mnaponza bure bosi wenu bila ya nyinyi kujijua na yeye kujijua, mkajikuta badala ya kumsaidia, mkamponza, Mzee Karma akamshukia kama mlivyomponza yule mtangulizi wake!. Thread 'Karma is Real na ipo Kweli. Everything Happens for a Reason. Wasaidizi wa Rais Samia mna wajibu wa kumsaidia Rais na Serikali yake Kuepuka Bad Karma!' Karma is Real na ipo Kweli. Everything Happens for a Reason. Wasaidizi wa Rais Samia mna wajibu wa kumsaidia Rais na Serikali yake Kuepuka Bad Karma!
Ni ushauri tuu!.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…