Vote namba 20 ya Bajeti ina utakatifu gani dhidi ya katiba ya nchi?

Vote namba 20 ya Bajeti ina utakatifu gani dhidi ya katiba ya nchi?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Tumemsikia kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo bwana Zitto pale Mbagala Zakhem akitueleza Watanzania namna mambo ya ajabu yanayoendelea Bungeni.

Amesema kwa ufasaha kuwa kifungu namba 20 cha bajeti ambacho kina fedha za Takukufu, Usalama wa Taifa na matumizi binafsi ya Rais kimewekewa zuio na sheria za Bunge kutojadiliwa. Hivyo kinapitishwa bila kuhojiwa na hesabu zake zinapokelewa bila kujadiliwa.

Nimejiuliza, kifungu hiki namba 20 kina source gani ya fedha nje ya kodi zetu? Rais anapotueleza kuwa kodi zetu ni muhimu kuzihoji matumizi yake lakini hatuelezi kwamba kuna fedha haturuhusiwi kuhoji matumizi yake kwa sababu tunaingilia usalama wa nchi?

Kiukweli siyo jambo la busara hata kidogo kutaka kuwafahamu maafisa vipenyo kwa sababu za usalama wa nchi, lakini hatuwezi kuona ni busara kutokujua uhalali wa matumizi ya fedha zetu za kodi kwa taasisi hizo hususan TISS na TAKUKURU. Hizi mbinu za kujengeana hofu zinatoa nafasi kwa wasio waaminifu kutapanya rasilimali za taifa bila kuwajibishwa. Kama kuna maafisa vipenyo ambao wanakiuka viapo vyao na kuwajibishwa, je kuna utakatifu gani uliotukuka kwenye eneo la matumizi ya fedha? Tusisahau ike kashfa ya DEEP GREEN ambapo mpaka leo hakuna aliyewajibishwa kwa ufisadi ule. Ilisemwa bungeni kwamba fedha zilizopelekwa kwenye akaunti za Deep Green zilitumika kwa.masuala ya usalama wa Taifa...... kesi ikazimishwa hapo

Kifungu namba 20 pia kinahusika na matumizi binafsi ya Rais. Tunampenda na kumuenzi rais wetu. Pia tunamuomba aangalie hili jambo kwa kina. Yeye ni taswira ya Taifa na pia raia namba moja. Tunapenda kumuona akiishi kama mfano katika eneo la.matumizi. hatuwezi kumuona anatumia fedha vibaya pale anapokuwa anatoa fedha kwa wananchi wenye shida mbali mbali.

Pia tunajua kuwa kazi anayoifanya ni ngumu, hivyo kifungu hiki kimhusu yeye zaidi na siyo taasisi nyeti z serikali. Nashauri kifungu hiki ambacho ndicho msingi wa madaraka makubwa ya kimungu kwa rais kiwe na subsections ambapo kila section isimame kwa clarity yake yaani tusihoji matumizi binafsi ya Rais lakini mapato na matumizi ya TISS na TAKUKURU yawe bayana kwa ajili ya kuimarisha utawala bora na uwazi kwenye fedha za umma.

Ikiwezekana fungu la masuala ya ulinzi na usalama yatenganishwe na matumizi binafsi ya Rais kwa sababu tunajuaje endapo fedha hizo zilitumika ama zitatumika kukandamiza haki za binadamu na kuathiri usalama wa raia kama taifa ili kustawisha usalama wa taasisi kwa kivuli cha usalama wa taifa.

KATIBA mpya ituletee taasisi imara na siyo kuimarisha sheria zinazosimamia ofisi yenye mkuu mmoja ambaye anaweza akaja shetani kukalia kiti na nchi yote kugeuka jehanamu ya moto ambayo funza wake hawafi.

Enewei
Tujadili kwa kuzingatia umuhimu wa usalama wa nchi. Lakini tuangalie umuhimu wa kuondoa makandokando yanayopelekea taasisi zetu za muhimu kunyooshewa vidole.

Mshana Jr Retired Ushimen raraa reree Mchambuzi MALCOM LUMUMBA zitto junior Lucas mwashambwa Voice of Hope 2022 figganigga Nyani Ngabu Ex Spy EagleEyed
 
....matumizi ya TISS na TAKUKURU yawe bayana kwa....
Matumizi yakiwa bayana hiyo haitakuwa TISS Tena. Mtalazimika kutafuta TISS nyingine lengo hii ya Sasa mnayotaka kujua matumizi yake ifanye kazi mnazotaka kujua. TAKUKURU nayo sina uhakika kuwa ipo more independent kwa Sasa. Nikipata uhakika huo nayo matumizi yake yasihojiwe.

Ni ukweli mchungu.
 
Matumizi yakiwa bayana hiyo haitakuwa TISS Tena. Mtalazimika kutafuta TISS nyingine lengo hii ya Sasa mnayotaka kujua matumizi yake ifanye kazi mnazotaka kujua. TAKUKURU nayo kwa ilitakiwa kuwa more independent lakini kwa Sasa ni kama haina uhuru huo. Nayo ukipata uhuru kamili wa kufanya kazi matumizi yake yasihojiwe.

Ni ukweli mchungu.
Tuelimishabe kwa kina kwenye eneo hili.

Kuhoji kila kipengele cha matumizi ni suala ambalo kwa akili za kawaida inagoma.

Lakini kwa mfano walipangiwa bajeti ya Tshs bilion 20 na zilizopelekwa ni Bilion 12 kisha mrejesho Bungeni tunaambiwa zimetumika B 20

Hapo ndo shida ipo
 
Umeandika pumba tupu
Matumizi yakiwa bayana hiyo haitakuwa TISS Tena. Mtalazimika kutafuta TISS nyingine lengo hii ya Sasa mnayotaka kujua matumizi yake ifanye kazi mnazotaka kujua. TAKUKURU nayo sina uhakika kuwa ipo more independent kwa Sasa. Nikipata uhakika huo nayo matumizi yake yasihojiwe.

Ni ukweli mchungu.
 
Hilo ni tatizo
Sasa kwa nini tuache vyombo vyetu vya kitaasisi kubebeshwa tuhuma zisizo zao?

Angalia leo namna ambavyo tunawadhalilisha wanausalama kwa mambo ambayo yanafanywa na wahuni?
Kwa mfano, si rahisi kutofautisha TISS na Uslama wa ndani ya CCM maana kila kitu ni kama kinafanyika kwa ushirikiano. Nani analipia hayo yote.

Tunataka ujasusi wa kimaendsleo, kisayansi na kung'amua vihunzi vya kimataifa na namna ya kuvikwepa.

Bajeti ilenge kuboresha utendaji wa taasisi zetu na siyo kutumika kama kichaka cha wanaokwapua mali ya umma kisha zigo wanaangushiwa Takukuru na TISS
 
Nadhani cha sasa na kikubwa kilicho mbele yetu ni katiba mpya maana kila unalogusa lina makandokando ya kutosha . kuna mambo ukiyachimna kidogo tu unaweza kufa kwa pressure
 
Takukuru haina sifa ya kuwa kwenye hilo fungu waiondoe tu.

Ni kati ya taasisi ambazo hazina tija kabisa ambazo watu wanakula mishahara tu.

Ivunjwe maafisa wachache waadilifu waingie TISs , wengine wapelekwe idara nyingine za serikali.
 
Takukuru haina sifa ya kuwa kwenye hilo fungu waiondoe tu.

Ni kati ya taasisi ambazo hazina tija kabisa ambazo watu wanakula mishahara tu.

Ivunjwe maafisa wachache waadilifu waingie TISs , wengine wapelekwe idara nyingine za serikali.
Halafu inaleta ukakasi kuona TAASISI Nyeti zipo ktk fungu la matumizi binafsi ya Rais.

Je hili fungu pia linaakisi utendaji wa taasisi hizo?
 
Back
Top Bottom