Serikali tangu mchakato ulivyoanza naona imejikita sehemu moja tu ufundishaji hapa cha msingi kwa shule za msingi lazima walimu wapewe semina za kufundisha kwa weledi madarasa ya kwanza na la pili kusoma,kuandika na kuhesabu na mitaala iboreshwe kuwe angalau kitabu kimoja kinachokidhi maudhui kwa watoto sio suala la kukazania ufundishaji wa kipurure kwa darasa la saba,pia kuwepo na sheria ya lazima ya kuwarudisha wanafunzi ambao hawataweza KKK na mitihani ya kuingia darasa la tano upewe umuhimu kama mtoto hataweza kufaulu akariri.Upande wa kidato cha kwanza wanapoingia wapewe mtihani kwa ajili ya kujidhirisha kama wanafunzi hawakuchakachuliwa upande wa vitabu pia kuangaliwe utaratibu wa vitabu bora sio Kina Nyambari Nyangwine wanakaririsha watoto hakuna maudhui yyte hapo.kwa shule za kata mabweni ni muhimu sn kwani kuna watoto wengine kijijini wanatoka zaidi ya km 8 na kuwepo sheria ya uchangiaji wa chakula cha mchana.Upande wa walimu semina ziwepo hasa kwa mada zile ngumu na maslahi yaboreshwe ikiambatana na uwepo nyumba za walimu za kutosha.Pia uwepo wa vifaa vya kutosha vya kujifunzia na kufundishia hasa madarasani angalau hii kauli mbinu ya BRN inaweza kufanikiwa kwa asilimia 60
sawa naona mawazo ni mazuri ,serikali iangalie sana mahitaji wa waalimu kwa jumla pia wakuu wa shule wawajibike katika kusimamia waalimu wao.Jambo jingine ni nidhamu ya wanafunzi,bila nidhamu hakuna elimu.Pia serikali itoe muongozo wa vitabu maalumu kuwa ndio rejea za somo lakini ikiwa kila shule itakuwa na vitabu vyake uwezekano wa kufeli upo palepale.
Jamani hiyo ni Tanzania,Tanzania ipo vijijini sio mijini.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.