VPL: Ihefu FC 1-2 Simba SC Sokoine, Mbeya

Da Gladiator

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
1,641
Reaction score
2,646
Patashika ya ligi kuu Tanzania Bara VPL, kuanza leo Jumapili 06, Septemba 2020. Leo zitapigwa mechi sita(6) katika viwanja mbalimbali. lakini katika uwanja wa Sokoine kuna bonge la mechi kati ya Ihefu FC na Simba SC.

Je, Ihefu FC ama Simba SC kuibuka mbabe? Kaa nasi usikose ukahadithiwa. Kumbuka mtanange ni kuanzia saa 10:00 jioni.
Je, Leo mkurugenzi wetu mpya mrembo Barbara Gonzalez atakuwepo?!, Hakika anapendeza kuwepo katika klabu kubwa kama Simba SC. Karibu Bibie tunakuamini.

"Kulitaka mwana, kulipewa mwana".
#SimbaNguvuMoja.
#AnotherLevel.
===

Dakika 90 Uwanja wa Sokoine zimekamilika kwa mchezo kati ya Ihefu FC na Simba kumalizika kwa Simba kushinda mabao 2-1.

Mabao yalifungwa na John Bocco dakika ya 10 na la ushindi lilifungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 42.

Lile la Ihefu lilifungwa na Omary Mponda dakika ya 14 na Simba kufanikiwa kusepa na pointi tatu kwenye mchezo wa kwanza.

Ihefu walikwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wamefungwa mabao 2-1 ambapo Simba ilianza kufunga bao kupitia kwa John Bocco dakika ya 10 lilisawazishwa na Omary Mponda dakika ya 14.

Bao la pili kwa Simba lilifungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 42.

Ihefu ambayo imepanda daraja ipo kwenye ubora wake ambapo wamecheza soka la utulivu na kuwapa tabu mabingwa watetezi Simba.



 
Gemu Kali ya wiki hii ni Beberu Mudi vs Kigwa. Mashabiki wa mbumbumbu fc chondechonde msije kujaribu kuhoji 20b beberu asije akajiuzuru.
Karibu tumjadili Ihefu, anavyokula saba(7). Achana na Hizo siasa.
 
Naona wanenda KUCHEZA ndani ya magofu ya uwanja.

Toka nyerere upo vilevile uwanja wa sokoine tena umekaaa kushoto.

Why wasiulete uwanja wa ndege wa zamani.

Any way WATANI ZANGU KILA la KHERI.
 
Naona wanenda KUCHEZA ndani ya magofu ya uwanja.

Toka nyerere upo vilevile uwanja wa sokoine tena umekaaa kushoto.

Why wasiulete uwanja wa ndege wa zamani.

Any way WATANI ZANGU KILA la KHERI.
Ungemjua mmiliki usingekuja na hizo ndoto!
 
Priiiiiiiiiiii, mpira umeanza. Refa Martin Sanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…