Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Baada ya kuondoka na alama moja katika mchezo dhidi ya Kagera sugar juma lililopita, Gwambina hii leo ameambulia patupu baada ya kuruhusu kichapo cha bao 1-0 akiwa katika Dimba la nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting.
Goli la Ruvu shooting lilifungwa na F Ikobela 47'.
Na katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam KMC wamefanikiwa kuweka kibindoni alama tatu muhimu baada ya kumchapa Mwadui goli 2-1.
Matokeo haya yanajirudia kwa Mwadui baada ya kufungwa goli 2-1 na Biashara katika Dimba la Mwadui complex Juma lililopita.
Magoli ya KMC yamefungwa na E Mvuyekure 13' na C Ilanfya, huku goli la Mwadui likifungwa na D Richard 70'.