VPL: Mwadui yaendelea kushika mkia msimamo wa ligi kuu

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105

Baada ya kuondoka na alama moja katika mchezo dhidi ya Kagera sugar juma lililopita, Gwambina hii leo ameambulia patupu baada ya kuruhusu kichapo cha bao 1-0 akiwa katika Dimba la nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting.

Goli la Ruvu shooting lilifungwa na F Ikobela 47'.

Na katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam KMC wamefanikiwa kuweka kibindoni alama tatu muhimu baada ya kumchapa Mwadui goli 2-1.

Matokeo haya yanajirudia kwa Mwadui baada ya kufungwa goli 2-1 na Biashara katika Dimba la Mwadui complex Juma lililopita.

Magoli ya KMC yamefungwa na E Mvuyekure 13' na C Ilanfya, huku goli la Mwadui likifungwa na D Richard 70'.
 
Mwadui FC wamekosa kushuka daraja misimu miwili mfufulizo Safari hii hiki kikombe hawatakieupuka naamini wanashuka daraja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…