VPL tarehe 18/11/2017: Tanzania Prisons 0 Vs 1 Simba Sports Club uwanja wa Sokoine, Mbeya

VPL tarehe 18/11/2017: Tanzania Prisons 0 Vs 1 Simba Sports Club uwanja wa Sokoine, Mbeya

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Ligi Kuu ya soka Vodacom (VPL) Mji wa Mbeya leo utasimama kwa dakika 90, kupisha mtanange kati ya Tanzania Prisons 'Wajelajela' na Simba Sports Club 'Wekundu wa Msimbazi'.

Je nani kuondoka na pointi 3 muhimu leo? Basi usikose ukaambiwa, kuwa nasi hapa.

Kumbuka mechi hii itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 2 na kwa upande wa radio TBC Taifa itapeperusha matangazo ya mbungi hii kuanzia saa 10. 00 jioni.

Vikosi kwa upande zote tukianza na wenyeji wa mchezo huu, Tanzania Prisons;

Aron Kalambo, Michael Ismail, Laurian Mpalile, Nurdin Chona, James Mwasote, Jumanne Elfadhili, Salum Kimenya, Kassim Hamisi, Eliuter Mpepo, Mohamed Rashid, Lambart Sabiyanka.

SUB;

Hassan Msham, Hamisi Maingo, Salum Bosco, Freddy Chudu, Kazungu Mashauri, Leonsi Mutalemwa, Vedastus Mwihambi.

Na upande wageni Simba Sports Club

Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, James Kotei, Yusuph Mlipili, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassir, John Bocco, Mwinyi Kazimoto, Haruna Niyonzima.

SUB;

Emmanuel Mseja, Ally Shomari, Nicholas Gyan, Laudit Mavugo, Juma Luizio, Mohamed Ibrahim MO, Jamali Mnyate.

==>Vikosi vya timu zote mbili vinawasili katika uwanja wa Kumbukumbu Sokoine mjini Mbeya.
371d5699b06e65238d14490a91ca8779.jpg


==> Wakati wowote mpira utaanza hapa uwanja wa Sokoine.

0' Naam mpira umeanza Tanzania Prisons 0 - 0 Simba SC

7' Goo laaaa Mohamed Rashid upande wa Tanzania Prisons anakosa goal la wazi hapa, mpira umeanza kwa kasi hapa


15' Tanzania Prisons 0 - 0 Simba SC

30 ' Bado milango ni migumu hapa, Tanzania Prisons 0 - 0 Simba SC

==> 45' Mpira ni mapumziko hapa uwanja wa Sokoine ambapo mpaka sasa hakuna timu imepata bao. Tanzania Prisons 0 - 0 Simba Sports Club


1' Mpira umeanza kipindi cha pili hakuna mabadiliko kwa wachezaji pande zote mbili.


75 ' Tanzania Prisons 0 - 0 Simba SC

84' Goooooooooaal John Bocco anageuka na ndani ya D na kuachia shuti kali na kuiandikia Simba goli la Kwanza. Tanzania Prisons 0 - 1 Simba SC

90 ' Tanzania Prisons 0 - 1 Simba Sports Club

93' Mpira umekwisha hapa uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya, ambapo matokeo ni kwamba Simba Sports Club imeibuka mshindi wa goli moja likifungwa na Mshambuliaji John Bocco 84' ambaye alikuwa Captain siku ya leo dhidi ya Tanzania Prisons ambayo haikupata goli.
 
Kikos cha bilioni 1.3 vs kikos cha mia tisa itapendeza sana.
Hakuna la ajabu hapo.. Leo EPL ni kati ya Manchester City ambayo imetumia hela nyingi kusajili msimu huu na Leicester City ambayo imetumia hela kidogo lakini timu zote ziko EPL na ushindani wake ni mkubwa

Kwa hivyo narudia tena 'hakuna la ajabu hapo' this is Simba.
 
9' Simba wanapeleka mashambulizi makali hapa upande wa Tanzania Prisons
 
18' John Bocco apiga shuti kali linatoka nje ya goli, ilikuwa nafasi nzuri hapa
 
Back
Top Bottom