VPL vs Ndondo Cup ya Clouds

Darmian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
17,289
Reaction score
46,624
Wakuu mambo ni nini?

Hivi inakuaje bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inadhaminiwa na mtandao namba moja wa simu TZ yaani Vodacom apate Tsh 80m wakati mshindi wa Ndondo Cup yeye anavuta Tsh 20m?

Hizi sio dharau?.

It's high time kwa mdhamini mkuu wa ligi kumwaga pesa kidogo,au kama vipi tumwachie Azam kila kitu.
 
We unataka bingwa wa VPL apewe shingapi?
 
Vodacom inatoa mzigo kila mwezi kwa kila timu. Pia klabu inapata mapato kwenye Viingilio. Kwenye Ndondo viingilio anachukua Shaffih
 
Vodacom inatoa mzigo kila mwezi kwa kila timu. Pia klabu inapata mapato kwenye Viingilio. Kwenye Ndondo viingilio anachukua Shaffih
Kiasi gani voda watoa per month kwa kila timu mkuu?
 
Usilinganishe Vpl yenye udhamini wa bil 22 kwa mwaka na ndondo cup
 
ila voda bora wajiweke pembeni ata ikiwa azam premn league
 
Sio 80m tu, Vodacom anagharamia pia safari za team.
So mkuu roughly tunaweza kusema udhamini wa Voda ni wa thamani gani kwa mwaka?.

Na usafiri hizi timu nyingi mbona huwa zinaunga unga tu na mabasi ? Ukiacha kina Simba,Yanga na Azam
 
Ligi zote duniani kombe la ligi ni kama Bonus tu huwa na thamani ya kawaida tu kifedha,,, ila timu inaingiza mapato kwa vyanzo tofaut tofauti,,,,,
 
So mkuu roughly tunaweza kusema udhamini wa Voda ni wa thamani gani kwa mwaka?.

Na usafiri hizi timu nyingi mbona huwa zinaunga unga tu na mabasi ? Ukiacha kina Simba,Yanga na Azam
Ulikuwa ni wa bilioni 3 kwa mwaka sema hela ya mwaka wa mwisho wameshindwa kutoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…