Vuguvugu Katiba Mpya latikisa mtandao wa Twitter

Vuguvugu Katiba Mpya latikisa mtandao wa Twitter

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165

Vuguvugu Katiba Mpya latikisa mtandao wa Twitter​

TUESDAY JUNE 22 2021​


Summary

  • Watu wa kada mbalimbali nchini Tanzania ni kama wameanzisha vuguvugu la kudai Katiba Mpya kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuendelea na mchakato huo.
By Peter Elias
More by this Author

Dar es Salaam. Watu wa kada mbalimbali nchini Tanzania ni kama wameanzisha vuguvugu la kudai Katiba Mpya kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuendelea na mchakato huo.

Kupitia vuguvugu hilo lililopewa jina la “KatibaMpyaMovement”, wananchi wamekuwa wakitoa maoni yao tofauti kueleza umuhimu wa kuwa na katiba mpya hapa nchini na wameitaka Serikali kurejea mchakato huo.

Katiba Mpya ni moja ya ajenda za vyama mbalimbali vya siasa nchini kikiwemo Chadema na CUF ambavyo vimekuwa vikipigania mabadiliko hayo kuwa pamoja na kuwa rais atapunguziwa madaraka, haki itatendeka katika chaguzi.

Hata hivyo, Rais Samia Suluhu Hassan katika moja ya hotuba zake baada ya kuwaapisha aliowateua alitaja neno katiba kisha akasema “sijui nina maradhi gani na katiba, suala la katiba mpya lisubiri.”

Gervas Sulle ameandika katika ukurasa wake,”katika Tanzania tulihitaji katiba kwa nyakati mbalimbali kwa kuwa ni muhimu. Kwa sasa katiba mpya ya wananchi ni lazima na sio ombi kwa maendeleo ya Taifa letu.

Anayekataa Katiba Mpya anataka tubaki na mtazamo wa maendeleo wa 1977. Ni CCM tu wanahofu kwa maslahi yao ya kisiasa.”


Mwananchi mwingine, Kumbusho Dawson amenukuu maneno katika kitabu cha Hayati Benjamin Mkapa cha My Life, My Purpose akiandika, “Iundwe tume huru ya uchaguzi itakayokubalika na vyama vyote vya siasa ndio chachu hasa ya kulea na kukuza demokrasia nchini.”

Dk Chris Cyrilo amesema, “hakuna Katiba Mpya kwa njia ya amani. Hakuna CCM wapo radhi kwa chochote wabaki na katiba hii inayolinda maslahi yao ya kiutawala na kiuchumi. Natamani tunaotaka katiba mpya tuliweke hili akilini.”

Ntele Benjamin amesema, “wasomi wa vyuo vikuu wana wajibu mkubwa wa kuamsha umma kudai katiba mpya. Katiba mpya sio matakwa ya Serikali ni matakwa ya wananchi. Ni wakati sasa vyuo vikuu kutoka walipojifungia na kupaza sauti Kuhusu Katiba mpya.”
 
uzuri mama yetu anapitia mitandao na kuona kipi kinaongelewa sana
 
Kumekuchaaa[emoji817][emoji736][emoji1548][emoji312][emoji313]
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Pengine hawa wakubwa wanaona hatueleweki, tuachane na suala hilo kwanza; kuna pande la ardhi linaelekea kumezwa na kakisiwa kadogo.

Tudai uhuru wa hilo pande kwanza, halafu tuone hiyo katiba ya JMT kama itashindikana kubalika!
 
Itachukua muda mrefu sana kupata katiba kupitia Twitter. Watanzania wengi hasa vijijiji hawaijui hiyo Twitter, hivyo serikali haijali sana. Ni Imani yangu around mwaka 2030-2040 Tanzania utakua na katiba mpya. Na ifahamike asiyetaka katiba mpya ni CCM Kwani Kikwete alitaka kutuachia katiba mpya wahafidhina wa CCM wakamshinda nguvu. One day yes mapambano hayajawahi kuwa rahisi.
 
..Kwa maoni yangu Katiba mpya inatakiwa iandikwe kwa kuangalia mbele / mbali.

..Nadhani ni vema tukaandika katiba hiyo wakati wakati huu ambapo taifa lina amani na mshikamano.

..Tukisubiri mpaka tuwe na maandamano, mashinikizo, na ghasia, za madai ya Katiba mpya tutakuwa tumechelewa. Na tutakuwa hatujalitendea haki taifa letu.

..Katiba mpya iandikwe kwa manufaa ya Watanzania wote.
 
Back
Top Bottom