Dah....ebana huu wimbo umenikumbusha enzi hizo pale Mwenge karibu na kambi ya jeshi ya ujenzi....kulikuwaga na mgahawa/baa/klabu moja hivi ilikuwa inaitwa Tarakea....walikuwaga wanapika mtori wa nguvu....halafu walikuwaga wanauza na chibuku (hivi hii nayo inahesabika kama pombe ya kienyeji? lol)....yaani nikikumbuka enzi hizo hadi machozi yananilengalenga aiseee
Nimekunywa sana chibuku (tulikuwa tunanywea mavikombe flani hivi makubwa) pale huku wimbo huu ukidunda kwenye maspika...