Smartkahn
JF-Expert Member
- Jun 22, 2020
- 594
- 1,061
UTANGULIZI
Tanzania ni nchi yenye uwezo mkubwa sana(potential) uwezo ni uwezo uliotulia, nguvu iliyohifadhiwa, nguvu isiyotumika, mafanikio yasiyotumika, vipawa vilivyofichwa, uwezo uliofungwa.
Vyote ambavyo nchi inaweza kua lakini bado haijawa, yote ambayo nchi inaweza kufanya lakini bado haijafanya... Inaweza kufika umbali gani lakini bado haijafika... Inaweza kutimia lakini bado haijatimiza uwezo ni uwezo iliyofunikwa nguvu iliyojificha, (Understanding Your Potential by Myles Munroe, 1991, P. 21).
Tuchukulie mfano huu wa mbegu nikikuonesha mbegu niliyoishika mkononi na kukuulizi nimeshika nini mkononi mwangu bila shaka utanijibu kuwa nimeshika mbegu lakini anaefahamu asili na uwezo wa mbegu atanambia kuwa mkononi mwangu nimeshika msitu... Kwanini? Kwasababu katika kila mbegu kuna mti na katika mti kuna matunda yenye mbegu na katika kila mbegu kuna miti kila miti kunamatunda yenye mbegu na katika kila zile mbegu kuna miti hatimae msitu mkubwa. Tatizo litatokea kama hautoipanda ile mbegu utakuwa umezuia uwezo wa mbegu kufanyika msitu... Tafakari nini ingekuwa hatima ya Diamond platinumz kama asingejikita kwenye muziki!?

Chanzo, Google; picha ikionyesha mabadiliko ya mji kabla na baada.
Tanzania sio kisiwa tukiwa kama taifa linaloungana na mataifa mengine kuunda dunia, hatuna budi kufunguka ili kuendanana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia inayopelekea mapinduzi ya nne ya viwanda.
Chanzo, Google velatia. com. Picha ikionyesha mapinduzi ya viwanda.
>>Kutokana na kupanuka kwa ombwe kati ya mataifa yalioendelea na sisi tunaondelea, kasi kubwa yaongezeko la watu inayotusogeza katika changamoto ya Ajira pia mabadiliko ya tabia ya nchi, hatima yetu ni nini? Tutakua tumefilisika kimaarifa na hekima kama tukiendelea kukumbatia rasilimali huku tukiwa tunafahamu fika uwezo wa kuziendeleza kwa wakati na katika viwango stahiki hatuna.
>>Uchumi tunao ila tumeukalia, tangu tupate uhuru mpaka sasa asilimia kubwa ya rasilimali bado hutujazivuna, uwiano kati ya rasilimali na hatua ya maendeleo tuliofikia hairidhishi kabisa. Ni wakati sasa wa kuacha kuhatamia rasilimali kwa kigezo cha kuzilinda mpaka pale tutakapopata wataalamu wetu wa ndani, kwasababu teknolojia inahadilika kwa kasi sana tutaishia kua na wataalamu wasiomudu mabadiliko hayo na pengine rasilimali sisiwe na thamani tena kwani tunashuhudia watu wanahama kutoka kutumia mafuta kwenda kwenye umeme.
Chanzo, Google; dreams time. com, picha ikiwakilisha shauku ya kutaka mabadiliko.
Sasa sisi kama taifa wenye shauku kubwa ya kuliona taifa linapiga hatua kubwa za kimaendeleo, kwanza ni lazima tukiri na kukubali madhaifu tuliyonayo ndipo tutafakari namna ya kujikwamua kutoka kwenye hali hii.
YAFUATAYO NI MADHAIFU AU CHANGAMOTO KUU ZINAZOTUKWAMISHA KATIKA KULETA MAENDELEO NCHINI.
=========================>Ni dhahiri shahiri Tanzania imejaliwa rasilimali za aina mbalimbali na zinapatikana kwa wingi mno lakini tumegubikwa na changamoto zifuatazo.
1. Tumekosa (mtaji) kiasi cha pesa cha kuweza kutoshereza kuzivuna rasilimali tulizobazo kwa viwango na ufanisi mkubwa.
2. Asilimia kubwa ya watanzania sio wawajibikaji/wachapakazi/waliokosa weledi kiasilia ni wavivu wanaotekeleza majukumuyao kimazoea.
3. Watanzania kitaaluma wanaelimu duni wengi wao wamegubikwa na imani potofu uchawi, uganga na miujiza.
4. Asilimia kubwa ya watanzania ni wabinafsi /warafi(greedy) katika Mali za umma unaopelekea rushwa wizi na ubadhilifu kukithiri.
5. Asilimia kubwa ya watanzania ni hawana nidhamu na ni wanafiki, ni ngumu kwa mtanzania kufanya jambo sahihi katika wakati na mahali sahihi.
>Sasa basi kwa taifa ambalo watu wake asilimia kubwa wanakua wametawaliwa na sifa hizi, basi moja kwa moja watu inakuwa na dosari katika kuleta maendeleo kwa taifa. Kwasababu;
▶️Kwanza Taasisi na mashirika ya umma yatakithiri kwa rushwa kama tunavyoona Polisi, mahakama, vyuoni na vituo vya afya.

Chanzo, Facebook. DW kiswajili.
▶️Pili mashirika makampuni na Taasisi mbalimbali zitajiendesha kwa hasara kwasababu watumishi hawana elimu na weledi wa kutosha kazini haya tunayashubudia kwa watumishi wa serikalini katika sekta mbalimbali wakifanya kazi kimazoea pasipo ubunifu wowote.
Chanzo, Facebook, Miradi Ayo.
▶️Tatu asilimia kubwa ya viongozi na watendaji wa serikalini ni wabinafsi na warafi(greed) w anachukua na kutumia mali za umma kwa maslahi yao binafsi na familia zao huku wakiacha huduma za kijamii zikizolota na wananchi kukukosa huduma stahiki kwa wakati.
Chanzo, Facebook, DW Kiswahili.
Kwa kifupi hali kama hii tunaweza tukaielezea kwa ufupi kamba "penye miti hakuna wajenzi" na tumekuwa katika hali hii kwa muda mrefu ni wakati sasa umewadia wakuvunja hali hii STATASI KUO.
=========================
=========================
STATASI KUO (STATUS QUO) Ni nini?
Ni hali halisi tuliyonayo na tunaondelea kua nayo. Kwa kua hali tuliyonayo ni mbaya na haifai kwa maslahi mapana kwa taifa basi hatuna budi kuivunja na kuifutilia mbali.
NAMNA YA KUIVUNJA STATASI KUO YA TANZANIA ILI KUIFIKIA TANZANIA TUITAKAYO 2025-2050.
Chanzo, Google; dreams time. com.
Chanzo, Google; dreams time. com.
🔘Kwanza kabisa fikilia wazo hili kutoka katika kanuni za kifizikia kutoka kwa Bwana Isaac Newton alizozigundua mnamo karne ya 17.
1.Newton's First Law of Motion states that "An object at rest will remain at rest, and an object in motion will remain in motion unless external force is applied on it" (forbes. com by Abdo Riani).
Tafsiri yake katika lugha ya kiswahili ni kwamba "Kitu chochote Kilichokua katika hali ya utulivu kitaendelea kua katika hali hiyo hiyo ya utulivu, na kitu chochote kilicho katika hali ya mwendo kitaendelea kua katika hali hiyo hiyo ya mwendo isipokua hali hizo zitabadilika endapo nguvu kutoka nje itatumika.
Mfano; jiwe lililotulia tu mahali litaendelea kutulia hapo hapo labda kitokee kitu kitakacho lihamisha jiwe hilo kitu hicho chaweza kua nguvu ya maji upepo matetemeko ya arthi na hata binadamu kupitia shughuli zake. Pia vivyo hivyo kwa gari lililo kwenye mwendo litaendelea kua kwenye mwendo isipokua litaweza kusimama endapo tu kutakua na nguvu kutoka nje yakulizuia nguvu inaweza kua dereva amefunga breki mafuta yamekwisha ama limekwama katika kizuizi chochote kile.
Kwahiyo kupitia kanuni hii tunapata kutambua kua nguvu kutoka nje ndio mbinu pekee itakayotuamsha kama taifa na kua hai kutoka katika hali hii duni ya kimaendeleo tuliyonayo miaka nenda rudi (STATASI KUO).
Unaweza ukajiuliza kwani wenzetu waliwezaje(wazungu)? Ukweli ni kwamba mataifa yote yaliyofanikiwa duniani hapa tokea mwanzo mpaka sasa kwa namna moja ama nyingine wametumia kanuni hii, kivipi ni hivi mataifa ya ulaya yalikuwa yanawatu makini na wenye uwezo mkubwa kifikra (Akili) ila changamoto ikawa hawana rasilimali za kutosha kuweza kutosheleza mahitaji ya viwanda walivyo vianzisha hivyo ikawabidi watafute nguvu(rasilimali) kutoka nje ili kuweza kuendeleza shughuli za uzalishaji na maendeleo nchini mwao ndipo wakaja Afrika, Amerika na Asia kututawala(ukoloni),

Chanzo, Google, ramani ikionyesha mataifa yakivuna rasilimali kutakua Afrika na Amerika kipindi cha ukoloni.
Pia mataifa mengi ya Asia na Amerika yameendelea baada ya ukoloni kwa kutumia maarifa ya mataifa ya watawala wao kipindi cha ukoloni. Hii inanifanya nirejeree methali inayosema "penye miti hakuna wajenzi" inamaana na kwenye wajenzi hakuna miti, "sasa ndugu zangu tujiulize sawa tunamiti je tunafanyaje ujenzi bila wajenzi? Hatuoni wenzetu walikua hawana miti ila wanawajenzi iliwabidi waje kwetu wakakata miti wakaenda kujenga kwao, basi na sisi tukachukue wajenzi kwao waje tujenge pamoja huku kwetu.
View: https://youtu.be/51JQZLACRMY?si=lAbVc9eRbFdvkd_t.
NGUVU HIZO KUTOKA NJE ZA KUWEZA KUVUNJA STATASI KUO YETU KAMA KANUNI ILIVYOAINISHA NI;
(i) Kuwavutia na kuwaleta wawekezaji na wabia wenye wasifu bora ili waje kuwekeza na kuingia ubia/ushilikiano kwa makubaliano maalumu katika Taasisi sekta na mashirika mbalimbali nchini.
(ii) Kukopa mikopo mkubwa yenye riba nafuu kutuka katika Taasisi za kifedha duniani, katika jumuiya, na nchi tajiri
(iii) Kubinafisha viwanda mgodi mashamba kwa Makampuni binafsi yenye wasifu mzuri na ushindani mkubwa kimataifa.
(iv) Serikali kushilikisha sekta binafsi na asasi za kiraia zenye ubora wa viwango vya kimataifa katika sekta mbalimbali za uzalishaji na utoaji huduma nchini hususani katika huduma za kijamii.
(v) kuajili viongozi na watendaji wa kampuni Taasisi na mashirika kutoka katika taifa lolote duniani pasipo kujali tofauti zetu ilimradi tu huyo kiongozi au mtendaji anavigezo na ubora(wasifu) unatakiwa kufukiwa katika kampuni taasisi nna mashirika mbalimbali nchini. Tujifuze hata kupitia ligi yetu ya mpira Wa miguu bila kusajili wachezaji wa nje tungesubili sana.

NAMNA NGUVU KUTOKA NJE ZITAKAVYOCHOCHEA MAENDELEO KUTOKA KATIKA HALI HII DUNI NCHINI (STATASI KUO DUNI)
1.Nguvu hizi zitaiwezesha Tanzania kumudu gharama za uanzishaji uendelezaji na uendeshaji wa miradi ya kimkakati pasipo kuasiri shughuli nyingine za kuendesha nchi kama vile utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi, na miradi itamalizika kwa wakati bila kusuasua.
=>>Nguvu mahsusi itakayowezesha hili ni Mikopo ya kutosha yenye riba na masharti nafuu kutoka katika benki ya dunia (WB) shirika la fedha duniani (IMF) jumuiya za kikanda na hata nchi tajiri.
=>kiuhalisia bila mbinu hii sisi kama taifa hatuta songa mbele kwani hatuna fedha/mtaji wa kutosha kuweza kuazisha miradi mkubwa kama hii ya uchimbaji madini na nishati (gesi na mafuta) pia bandari kubwa na zakisasa na mitambo ya nyuklia.
2.Nguvu hizo zitatuletea teknolojia na ujuzi wa kisasa katika sekta mbalimbali za uzalishaji na utoaji huduma, pasipo kutimia gharama wala muda mrefu kupata kama tukipambana wenyewe kwasababu tunashirikiana na wamiliki wenyewe wenye teknolojia yao kupitia;
=>>Uwekezaji ubinafsishaji na ubia baina ya Makampuni ya ndani na ya nje ya nchi zilizoendelea kama Japan China Korea Germany ama Marekani, kupata wabia wawekezaji kama hawa inamaana moja kwa moja watasafirisha ujuzi na teknolojia yao na kuisimika huku kwetu ndio tunakua tumeshapata teknolojia mpya na yakisasa.
=>Kiuhalisia sisi wenyewe hatuna uwezo wa kumudu gharama za teknolojia na ujuzi wake na namna ya kutunza na itatughalimu muda mrefu na nguvu/pesa kubwa mno kuweza kupata teknolojia na hatuna nchi utakayo tupatia maarifa na teknolojia bure wanaishia kutupa msaada ambayo kiuhalisia haitusadii inatufanya tuwe tegemezi, msaada ya chakula na vifaa tiba. Iliwapasa "watufundishe kuvua samaki na sio kutupatia samaki" hii yote ni kwasababu "mkono mtupu haurambwi" inatakiwa tufungue mipaka yetu kama nchi.
3.Nguvu hizi zitatuwezesha kua na ushindani baina ya sisi wenyewe ndani ya nchi na kati yetu na mataifa makubwa duniani, kwani ufanisi wa uzalishaji bidhaa na utoaji huduma utakua kwa kasi na viwango vya juu vya kuweza kuleta ushindani katika soko la kimataifa. Pia ushindani huu utapelekea Taasisi kampuni na mashirika katika sekta mbalimbali kuacha kufanya kazi kimazoea automatiki zitajikuta katika ushindani wa kuzalisha bidhaa na utoaji huduma bora ili kulinda/kuendelea kutawala soko, Kwahiyo ufanisi utaongezeka maradufu pasipo hata usimamizi wa serikalini kutumia nguvu ya sera na sheria kuhimiza.
=>>Kwahiyo kupitia kuwaleta wawekezaji wabia na ubinafsishaji kwa kampuni zilizo na sasifu mzuri na kutoka katika mataifa yanayosifika kwa uchapakazi na weledi duniani watakuja kutuambukiza hali hiyo kwa muda mfupi sana.
=>Kiuhalisia kwa hali hii tuliyonayo (statasi kuo) Tanzania hatuwezi kuleta ushindani ama kushinda huko kwenye soko la dunia hususani katika kutoa bidhaa na huduma bora kama tutaendelea kufanya mambo kibinafsi inatakiwa tufunguke sisi kama nchi kwani wenzetu wamepiga hatua kubwa zaidi mapinduzi ya nne ya viwanda hivyo njia rahisi ya kuendanana na kasi hiyo ni kushirikiana ni lazima tufungue nchi kwani "mkono mtupu haurambwi"
4.Nguvu hizo zitaongeza na kuimarisha maradufu uwajibikaji wa Watumishi wa umma mashirika Taasisi na wajasiriamali kwa ujumla, azaki na hata viongozi wa serikalini. Uwajibikaji unaohusisha uchapakazi kwa weledi na ubunifu.
=>>Kiuhalisia hari tuliyonayo kiutendaji/uwajibikaji wa aidha viongozi watendaji ama watumishi wa umma ni tatizo kubwa sana tena sana na nikilio cha muda mrefu, ni kweri mashirika Makampuni taasisi zinaendeshwa kwa hasara miaka nenda rudi, kutokana na kukosa uwajibikaji weledi na ubunifu unapelekea sekta hazikui katika uzalishaji bidhaa na utoaji huduma bora, kinyume chake kumekithiri vitendo vya wizi rushwa na ubadhilifu wa mali za umma.
=>Sasa basi kupitia nguvu za nje kama vile kuingia ubia na makampuni ya nje, ubinafsishaji na Uwekezaji katika sekta mbalimbali kuajiri viongozi na watendaji wa makampuni wenye vigezo bora zaidi kwa kuwashindanisha wasifu wao basi tutakua tunatatua tatizo kwani jamii mpya hii ya watu itachagiza uchapakazi weledi ufanisi na uwajibikaji kwa wazawa waliozoea kufanya kazi kimazoea.
5.Nguvu hizo zitaingezea Tanzania mtandao mipana na yauhakika ya masoko na wadau katika sekta mbalimbali kutoka mataifa mashuhuli katika nyanja tofauti tofauti duniani.
=>>Kwasababu wabia wawekezaji azaki makampuni na mashirika tunayoingia makubaliano maalumu kufanya shughuli mbalimbali nchini yana uwezo na uzoefu wa muda mrefu na yana mtandao imara wa wadau na wateja(masoko), hivyo basi tutakapo waharibisha na kushirikiana nao inamaana mtandao wao wa wadau na masoko yaliyo wagharimu muda na mali kuyatengeneza yanakua ni yetu pia pasipo kuingia gharama walizoziingia wao.
=>Lakini hali halisi jinsi ilivyo na kwa kutumia nguvu zetu pekeetu itakua sio kazi rahisi kupata ushawishi wa hao wadau na masoko, itatughalimu muda mrefu na gharama kubwa mno kuwafikia na pengine tusifanikishe kabisa kwani ushindani ni mkubwa na isitoshe hatuna ubora/viwango vya kukaa ligi moja nao, hivyo hatuna budi kushirikiana nao.
6.Nguvu hii itatusaidia kuvunja (statasi kuo) ile mifumo na mnyororo mzima wa wizi rushwa na ufujaji wa mali za umma uliojikita mizizi katika mashirika ya serikalini, mfano mifumo ya wizi bandarini, mamlaka ya mapato, ardhi, uhamiaji nakadhalika.
=>>Kupitia wawekezaji wabia ubinafsishaji na kuajiri watendaji kutoka nje itasaidia kuboresha mfumo mzima wa shirika ama Taasisi kampuni hivyo ile mizizi ya wizi haitabaki salama pia kutakua na matumizi ya mifumo mipya inayotumia teknolojia ya kisasa itakayo Punguza mianya ya wizi rushwa na ubadhilifu ukilinganisha na mifumo analojia tulionayo.
=>Kuifikia Tanzania tuitakayo hatuna budi kuchukua hatua hizi kwani wizi ubadhilifu na rushwa vitatukwamisha sana kwani wezi tunawafahamu ni wazawa wenzetu na kuwadhibiti ni ngumu kwani ni umekua mtandao mkubwa ndani ya mfumo hivyo basi tujitahidi kubadiri mfumo, na hawatakubali kiurahisi mifumo kubadirishwa hivyo tunauhitaji kukaza mkanda na buti safari bado mbichi.
7.Nguvu hizi zitaipunguzia serikali mzigo wa majukumu kwa ile bajeti iliyotakiwa itegwe kwenye sekta mathalani katika usafirishaji basi inahamishiwa matumizi na kwenda kwenye elimu ama afya kwani huku kwenye usafirishaji kuna sekta binafsi azaki kampuni walioingia ubia na uwekezaji wengine wamebinafsishiwa hivyo wanatumia mitaji yao.

HITIMISHO
Hayo yote yaliyoainishwa hapo juu kwa ujumla wake hayawezi kitimia bila kua na uongozi mzuri nchini inatakiwa safu nzima/yote ya viongozi kuanzia serikali kuu mpaka serikali za mitaa kua imara, Ninaposema kua imara namaanisha kua na viongozi wenye uthubutu na maamuzi magumu kwanini maamuzi magumu kwasababu kuna watu wanaenda kinyume na sheria za nchi wananguvu na uishawishi na wamejipanga wanapokua wanatekeleza maovu yao ndani ya nchi(yaani wanaijua sheria vizuri na kucheza nayo). Sasa kama kiongozi ukisema ufuate sheria kwa watu wa namna watakuchezea sana na kupoteza muda wa kushughulika na mambo mengine.
Uongozi imara ndio utakao simama kwa makini fedha zetu tulizozipata katika kodi na mapato ya ndani na nje bila kusahau Fedha za mikopo na msaada.
Pia ulinzi na usalama wa taifa uimalishwe maradufu tukiwa tunaondelea kuwaleta wawekezaji, wabia na watendaji mbalimbali kutoka mataifa tofauti tofauti duniani hutuwezi tukajua dhamira ya kila mgeni wengine wanaokuja wa madhumuni zaidi ya moja tofauti na kilichowaleta, hivyo nitoe rai yangu kwa mamlaka kulitizama hili kwa jicho la tatu kuanzia mipakani angani ardhini majini mtandaoni na ubarifu wa kibiolojia pia pasipo kusahau uhandisi jamii.

Chanzo. Google, https://www.act.nato.int/article/mdo-in-nato-explained/[/I].
Upvote
1