Kwa ukweli inashangaza kuona chama kikongwe kimekuwa kikihubiri wapinzani kukubali matokeo. Hali ikionekana inakula kwao, basi wao wanakuwa wa kwanza kutokukubali kupokea matokeo! Hii imethibitika maeneo kama ya arusha, mwanza, hai, na sasa mbeya. Lakini maeneo ambayo chama hicho kikongwe kimeshinda, aaa, hamna shida, matokeo yametangazwa fasta.
Sasa mpaka watu washinde na njaa, walale barabarani, wachome moto ndo wanalazimika kutangaza matokeo.
Unafiki huu haufai. Inakera. Wapinzani watakapoingia bungeni, kweli waweke nguvu ya kuwepo tume huru ambayo wakati wote haitajiona kana kwamba wameajiriwa na chama twawala.