Muktadha: Wakati mchakato wa kuhesabu kura kuwapata viongozi wapya wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) ukiendelea, baadhi ya wanaodaiwa kuwa makada wa chama hicho wanashikiliwa na polisi kwa madai ya kuanzisha vurugu.
Tukio hilo limetokea leo Ijumaa, Januari 17, 2025 wakati kura za wajumbe wa mkutano mkuu, baraza kuu, na viongozi wa Bawacha zikihesabiwa katika ukumbi wa mikutano wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa wafuasi hao walianzisha vurugu wakitaka kuingia ndani ya uzio wa ukumbi huo, lakini hawakuruhusiwa kwa sababu si wahusika wa mkutano huo, hatua iliyozua mvutano kati yao na walinzi waliokuwa eneo hilo. Mwananchi limeshuhudia askari polisi wapatao sita wakiingia kwenye korido za ukumbi huo kupitia mlango mwingine na kwenda moja kwa moja nje ya uzio wa ukumbi kuwakamata wanaodaiwa kuanzisha vurugu na kuondoka nao.
Your browser is not able to display this video.
Vurugu zimeanzishwa na wanaume wanaodaiwa kurandaranda nje ya ukumbi walipo wapigakura.