Vurugu zinazotokea Zanzibar: Sina imani tena na Prof Baregu katika mchakato huu wa katiba mpya

Vurugu zinazotokea Zanzibar: Sina imani tena na Prof Baregu katika mchakato huu wa katiba mpya

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2009
Posts
2,653
Reaction score
266
Akizungumza na NIPASHE jana, Kamishina wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu, alithibitisha kuvunjika kwa mkutano huo kwa mara ya pili baada ya kutokea vurugu na mabishano makali baina ya wananchi kabla ya Tume kuanza kazi ya kukusanya maoni.

Aidha, alisema kwamba watu hao ambao siyo wakazi wa maeneo husika wamekuwa wakitaka mfumo wa Muungano wa serikali tatu ikiwamo ya Muungano wa mkataba, lakini wamekuwa wakifanya vitendo vya vurugu kama kushangilia na kuzomea kwa watu wanaotoa maoni tofauti na mtazamo wao jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa ukusanyaji wa maoni.
Kamishina huyo alisema hafahamu kama wananchi wanaopelekwa kwa magari kutoa maoni kama hawana nauli au katika maeneo wanayoishi hakuna huduma za kawaida za usafiri kama daladala, lakini alisema ni kosa kwa mwananchi kutoa maoni zaidi ya mara moja kwa mujibu wa sheria.





KWANINI SINA IMANI NA PROF BAREGU?

Haijui CCM? hawajui ccm walivyomhujumu DK SLAA? haijui tume ya Uchaguzi? Kwa hivyo wakati yeye anampigania dk Slaa hakujua Mbinu za CCM?
Kwanini asiwalaumu CCM hukO zanzibar badala yake anawalaumu wapinzani?


SOMA HAPA PIA UONE UDHAIFU WA PROF BAREGU


[h=1]HALI INAZIDI KUTISHA MCHAKATO WA UTOAJI MAONI ZANZIBAR[/h]Written by Ahmed Omar Khamis // 12/12/2012 // Habari // 3 Comments


• CCM wanaufanya mchakato ni wao, mali yao.
• Serikali inawapa uso kutekeleza vitimbi viovu dhidi ya mchakato huo.
Utowaji wa maoni katika wilaya ya Mjini ratiba imepanga vituo vyote vya kutoa maoni jirani na matawi imara ya CCM ili kutoa urahisi kwa CCM kuuteka nyara
mchakato katika wilaya hii. Wakiwa katika matawi yao hayo kiasi cha wanachama 70 hivi hulala hapo tawini huku wakigharamiwa magodoro ya kulalia na vyakula. Kama hilo halitoshi CCM hulazimisha kutumika kwa vifaa vyao vya jukwaa na viti vya kukalia. Mara wakifika katika eneo la kutoa maoni hupanga viti vyao na mabenchi kwa utaratibu wao na kukalia viti hivyo. Baadhi ya viti hua vitupu na huwekwa ili kuwazuilia nafasi wenzao watakapokuja baadae. Haya ndio yaliyojitokeza leo asubuhi katika shehia ya M/Matarumbeta Jang’ombe.Hata hivyo wananchi ambao walidhaniwa kuwa ni wafuasi wa mkataba walifukuzwa na kupigwa huku wakiambiwa wende Pemba wakatoe maoni M/Matarumbeta pana wenyewe.
Baada ya wanamkataba kuchachamaa sheha akishirikiana na wana CCM walipiga simu polisi na ghafla gari mbili za FFU zilifika. Mara baada ya kufika waliwasikiliza wana CCM madai yao na ndipo wao waliposaidia kuwasogeza nyuma zaidi wanamkataba. Vijana wawili walijaribu kugoma na kuhoji kwa nini polisi wanafanya hivyo lakini walisombwa na kuingizwa katika defennder na kuchukuliwa na pingu mikononi.
 
Back
Top Bottom