Vuvuzela "huenda inaeneza maradhi"

Vuvuzela "huenda inaeneza maradhi"

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Upulizaji kidogo tu wa Vuvuzela hutoa mate mengi sawa na yanayotoka wakati mtu akipiga chafya, yakisafiri kwa mwendo wa kasi ya mara milioni nne kwa sekunde moja kwa kila tone, hii ni kwa mujibu wa jarida la PLoS One.

Katika eneo lililofurika watu, mtu mmoja akipuliza vuvuzela linaweza kuwaathiri watu wengine wengi kwa magonjwa yanayosambazwa kwa kuvuta hewa kama mafua na kifua kikuu.

Waandalizi wa michezo ya Olympiki mjini London mwaka 2010 bado wanafikiria iwapo waruhusu vuvuzela kutumika au la.

Dr Ruth McNerney, aliyeendesha utafiti wa hivi karibuni katika shule inayohusika na masuala ya usafi na maradhi ya nchi za joto ya London - London School of Hygiene & Tropical Medicine, amesema "upulizaji wa chombo cha vuvuzela" huenda kinahitajika kuliko kukipiga marufuku.

"Kama ilivyo wakati wa kukohoa na kupiga chafya, hatua zinapaswa kuchukuliwa kuzuia uenezaji wa maradhi, na watu wenye maradhi ya kuambukiza washauriwe wasipulize vuvuzela zao karibu na watu", alisema.

Kamati yake iliyochunguza hatari zinazoletwa na upulizaji wa vuvuzela, waliwatumia watu wanane waliojitolea kupuliza vuvuzela.

Kwa wastani chembechembe zinazotoka kwenye mapafu, 658,000 kwa lita ya hewa zilitolewa kutoka kwenye vuvuzela.

Matone hayo ya mate yaliruka angani kwa kiwango cha mara milioni nne kwa sekunde.

Kwa kulinganisha, wakati watu hao waliojitolea walipotakiwa kupiga kelele, waliweza kutoa mate kiasi cha chembechembe 3,700 tu kwa lita kwa kiwango cha 7,000 kwa sekunde.Upulizaji kidogo tu wa Vuvuzela hutoa mate mengi sawa na yanayotoka wakati mtu akipiga chafya, yakisafiri kwa mwendo wa kasi ya mara milioni nne kwa sekunde moja kwa kila tone, hii ni kwa mujibu wa jarida la PLoS One.

Katika eneo lililofurika watu, mtu mmoja akipuliza vuvuzela linaweza kuwaathiri watu wengine wengi kwa magonjwa yanayosambazwa kwa kuvuta hewa kama mafua na kifua kikuu.

Waandalizi wa michezo ya Olympiki mjini London mwaka 2010 bado wanafikiria iwapo waruhusu vuvuzela kutumika au la.

Dr Ruth McNerney, aliyeendesha utafiti wa hivi karibuni katika shule inayohusika na masuala ya usafi na maradhi ya nchi za joto ya London - London School of Hygiene & Tropical Medicine, amesema "upulizaji wa chombo cha vuvuzela" huenda kinahitajika kuliko kukipiga marufuku.

"Kama ilivyo wakati wa kukohoa na kupiga chafya, hatua zinapaswa kuchukuliwa kuzuia uenezaji wa maradhi, na watu wenye maradhi ya kuambukiza washauriwe wasipulize vuvuzela zao karibu na watu", alisema.

Kamati yake iliyochunguza hatari zinazoletwa na upulizaji wa vuvuzela, waliwatumia watu wanane waliojitolea kupuliza vuvuzela.

Kwa wastani chembechembe zinazotoka kwenye mapafu, 658,000 kwa lita ya hewa zilitolewa kutoka kwenye vuvuzela.

Matone hayo ya mate yaliruka angani kwa kiwango cha mara milioni nne kwa sekunde.

Kwa kulinganisha, wakati watu hao waliojitolea walipotakiwa kupiga kelele, waliweza kutoa mate kiasi cha chembechembe 3,700 tu kwa lita kwa kiwango cha 7,000 kwa sekunde.
 
Back
Top Bottom