Vx moja ya Serikali iuzwe ili kufanyia matengenezo hili Daraja

Vx moja ya Serikali iuzwe ili kufanyia matengenezo hili Daraja

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Mbunge wa jimbo la Ulanga Salim Alaudin Hasham ametembelelea katika kata ya Mwaya kujionea uharibifu uliojitokeza wa daraja kuvunjika na kusababisha kata nne za Mwaya, Ilonga, Mbuga na Ketaketa kukosa mawasiliano

Mbunge Salimu amesema kwa sasa ameishatoa taarifa ya changamoto hiyo kwa mamlaka husika na hatua za haraka zitachukuliwa huku akiwapongeza wananchi kwa kujitolea michango ya fedha kiasi cha shilingi 1,200,000 kwa ajili ya kivuko cha muda naye tayari ametoa kiasi cha fedha shilingi 1,000,000 huku Mwenyekiti wa Halmashauri akichangia kiasi cha shilingi 300,000 na jumla kupatikana kiasi cha shilingi 2,500,000

Pia Mbunge Salimu amewataka wananchi kushirikiana na wataalamu katika ujenzi wa kivuko hicho cha muda kipindi ambacho anaendelea kupambana kupata daraja imara ili kuweza kurejesha huduma za kijamii kama awali

Screenshot 2024-02-09 100855.png
 
Wanasubiria kuja kulitengeneza na msafara ili walizindue na bajeti ya billion moja wakat wametumia mbao
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Wabunge wanataka pesa ya Tanzania iwe na picha ya Rais Samiah. Hayo mambo ya daraja mtajua wenyewe.
 
Back
Top Bottom