SoC02 Vya kale vya dumisha vya sasa vya dhoofisha

SoC02 Vya kale vya dumisha vya sasa vya dhoofisha

Stories of Change - 2022 Competition

Kaka Ibrah

Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
83
Reaction score
65
Kulingana na mada kama jinsi nilivyo itambulisha hapo juu "VYA KALE VYA DUMISHA VYA SASA VYA DHOOFIDHA", hapa nazungumzia juu ya suala la "Afya".

Baadhi yetu wapo ambao wamekuwa wakiamini kuwa afya ni kuwa na mwili ulionenepa, pia wapo ambao wanaamini kuwa afya ni kuwa na muonekano mzuri (mvuto) wa sura, kitu ambacho si kweli. Bali; Afya ni hali ya mwili kujengwa ama kuwekwa katika hali ya matunzo kwa kufuata kanuni bora za lishe, chanjo dhidi ya magonjwa na kuzingatia mazoezi.

Hali ya sasa ya kiafya ya watu wengi imedhoofika ukilinganisha na ile ya mababu na mabibi zetu walio tutangulia kuishi hapo awali. Hii imechangiwa na mambo mengi ya kiikolojia lakini hasa zaidi ni kutokana na aina ya matumizi ya vyakula. Mababu zetu walitumia zaidi vyakula vya asili kama vile ugali dona, ugali wa uwele, ugali wa mtama, ugali utokanano na unga wa mihogo, wali, vyakula vitokanavyo na jamii ya mikunde kama vile maharage, kunde, mbaazi, choroko, dengu. Lakini menyu zao ziliambatana zaidi na mbogamboga kama vile majani ya maboga (yaani pitiku au msusa), uyoga, mgagani, mchicha, majani ya kunde (yaani nsansa), mlenda, nakadharika. Aina ya vyakula kama hivi vya asili huwa imara zaidi katika kujenga mwili wa binadamu na huupa mwili kinga yake dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Kale-768x424.jpg

Chanzo cha picha; thewitchkitchen.com
(Mboga ya majani aina ya sukuma wiki ikiwa imekomaa vizuri tayari kwa kupikwa na kutumiwa kama mboga yenye vitamin E kwa wingi).


IMG-20141211-WA0007.jpg

Chanzo cha picha; ruhuwiko.blogspot.com
[Mkusanyiko wa vyakula vya aina tofautitofauti (ugali wa mtama, ugali wa uwele, dagaa, mchuzi wa nyama, samaki na mswalu/itokanayo na majani ya maboga) ukitengeneza lishe iliyo kamili kwa afya ya mwili na akili ya mwanadamu].


Janga kubwa la kiafya linaukumba kalibu ulimwengu mzima kwa kizazi cha sasa. Matumizi ya vyakula vyenye mlundikano wa kemikali yameongezeka, mbaya zaidi tumelifanya swala la kufanya mazoezi kuwa ni kama la ziada. Matumizi ya vileo yamekuwa ni makubwa. Pombe, bangi, mirungi, miraa, madawa ya kulevya na uvutaji wa sigara pia yameathiri sana afya za walio wengi. Hali hii imepelekea miili yetu kuwa dhoofu na kushambuliwa na maradhi kwa wepesi, kitu ambacho kimepelekea kupungua kwa kiwango chetu cha kuishi miaka mingi ukilinganisha na wazee wetu wa zamani ambao hawakutumia vitu hivi.

10.jpg

Chanzo cha picha; clcl.ru
(Aina ya vinywaji vyenye kemikali hatarishi ambavyo hupelekea kudhoofisha mwili wa binadamu).

fb-nut-milks-promo.jpg

Chanzo cha picha; globalpublishers.co.tz

10-health-benefits-honey-3.jpg

Chanzo cha picha; www.pamperedpeopleny.com
(Picha ya maziwa na asali hapo juu ni moja kati ya aina ya vyakula vinavyo dumisha mwili na kuupatia afya yake na kuweza kujitengenezea kinga mwili ya kutosha dhidi ya magonjwa).


Neema ya nchi tuliyo achiwa na Mwenyezi MUNGU bado haijaondolewa. Tumezungukwa na mazingira yenye vitu vingi ndani yake ambavyo vya faa kwa matumizi ya mwanadamu katika kuijenga na kuimalisha afya yake. Mfano; matunda pori na matunda ya kupandwa. Matunda pori kama vile ntalali, fulu, na matunda ya kupandwa ambayo kalibu kila mtu ayafahamu, ambapo mtu awaye yote aweza kutumia kwa ajiri ya kujenga mwili na kuimalisha afya yake.

FUZ9yl0WYAEvkET.jpg

Chanzo cha picha; twitter.com
(Tunda aina ya fursadi likiwa tayari kwa kuliwa na kuongeza vitamin C ndani ya mwili wa binadamu).


Wakati mwingine si vyema sana kukimbilia madawa ya kisasa kila unapo umwa, yapo magonjwa ama maradhi mengine ambayo mtu aweza kujitibu kupitia madawa ya miti shamba na akapona kabisa. Mfano; mafua, kikohozi, madonda koo na kidonda. Kuna miti ambayo inaitwa "mifubata" ambayo majani yake kutumika kutibu kidonda. Aina hii ya miti inapatikana zaidi mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Katavi. Asali na tangawizi hutibu kikohozi, maji ya miwa hutibu tumbo la kuhara, nakadharika.

Zipo jamii ambazo hapa nchini zimepiga hatua katika kuzingatia matumizi ya vyakula na madawa ya asili zaidi, jambo ambalo limekuwa ni lenye manufaa kwao. Mfano; jamii ya kimaasai ndiyo jamii pokee yenye wazee wengi zaidi hapa nchini, na ndiyo jamii ambayo watu wake kuishi zaidi katika takimwi ya nchi. Yote hii ni kutokana na kwamba wanaamini zaidi katika vyakula vya asili kama vile asali, maziwa, ugali, wali, makande, chakula chenye mchanganyiko wa maziwa, mahindi, ndizi mbichi, viazi mviringo na chumvi (yaani loshoro) pia kujitibu maradhi madogomadogo kwa kutumia madawa ya miti shamba.

hqdefault.jpg

Chanzo cha picha; DW Kiswahili

Afya ya mtu haiwezi kukamilika iwapo usafi wa mtu binafsi pamoja na mazingira yanayo mzunguka haufanyiki. Swala la usafi lina nafasi kubwa katika kudumisha afya mtu. Usafi ukifanyika vyema inasaidia kumkinga mtu dhidi ya magonjwa ya mlipuko kama vile magonjwa ya kuhara, kipindupindu na homa ya matumbo. Mazingira ya nnje ya nyumba ni muhimu yasafishwe vizuri, ndani pia choo ni lazima vifanyiwe usafi tena kwa sabuni, maji mengi na madawa ya kuulia vijidudu kama vile mende na bakteria.

Kwa mantiki hiyo tunaona kwamba; ili kuijenga miili yetu na kuifanya iwe na afya njema, ni lazima tule chakula bora, tule matunda kwa wingi, tuzingatie matumizi sahihi ya dawa pindi tunapo ugua kwa kufuata maelekezo ya wauguzi, tutunze na kusafisha mazingira yetu ikiwa ni sambamba na usafi wa mtu binafsi. Vilevile pia tukumbuke kufanya mazoezi mala kwa mala ili kuinusulu miili yetu dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu na kukumbwa na matatizo ya visukuli ambayo ndio yamekuwa yakikatisha uhai wa watu walio wengi katika zama hizi. "Vya kale vya dumisha vya sasa vya dhoofisha".

_115586474_kegels.jpg

Chanzo cha picha; www.worldpress.com
(Mazoezi ya viungo vya mwili husaidia kuujenga mwili vizuri na kuifanya akili kukua vyema, pia husaidia kuukinga mwili dhidi ya magonjwa kama vile kisukari na shinikizo la damu).



Shukrani za dhati kwa kila mmoja, nawasilisha.
 

Attachments

  • _115586474_kegels.jpg
    _115586474_kegels.jpg
    14.6 KB · Views: 4
Upvote 0
Back
Top Bottom