VYAKULA NA MAGONJWA; Faida na hasara ya unga wa mahindi wa kukoboa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KWA UFUPI

  • Kwa sababu, hawataweza kula chakulacha cha kutosha na kupata virutubisho hasa wanga kwa kiasi kinachohitajika na mwili. Kinachotakiwa ni kuwaelimisha njia mbadala ya kuziba pengo la virutubisho linaloweza kupatikana na matumizi ya unga uliokobolewa.

Mara nyingi baadhi ya watu huwahimiza watu wengine kutumia unga wa mahindi au nafaka zingine usiokobolewa bila ya kubainisha hasara ya unga wa aina hiyo.

Watu wengi katika baadhi ya mikoa hawako tayari kutumia unga usiokobolewa. Kuwalazimisha watu wa aina hiyo kutumia unga usikobolewa (unga wa dona) ni sawa na kuwaweka watu hao katika hatari ya kuwa na lishe duni.

Kwa sababu, hawataweza kula chakulacha cha kutosha na kupata virutubisho hasa wanga kwa kiasi kinachohitajika na mwili. Kinachotakiwa ni kuwaelimisha njia mbadala ya kuziba pengo la virutubisho linaloweza kupatikana na matumizi ya unga uliokobolewa.

Unga wa mahindi

Unga wa mahindi ni chanzo kikubwa kwa watu wengi barani Afrika cha virutubisha kama vile wanga, protini, madini na vitamini. Hata hivyo, namna ya usagaji na matumizi ya unga wa mahindi yanaweza kuukosesha mwili faida ya virutubisho vilivyomo katika nafaka hiyo.

Unga wa dona na ule uliokobolewa

Mahindi au nafaka zingine zikikobolewa hupoteza sehemu fulani ya nafaka hizo. Kama mahindi yatasagwa bila kukobolewa unga wake huitwa unga wa dona (whole-grain flour). Na unga uliokobolewa kwa lugha ya kigeni unaitwa "refined flour".

Kwa upande wa mpunga kama utaondolewa ganda lake gumu la nje na bila kuungarisha, mchele huo kwa kimombo utaitwa "brown rice". Na kama utangarishwa zaidi unatitwa "polished rice".

Faida ya unga wa dona

Unga wa dona ni unga usiokobolewa. Aina hii ya unga unafaida kaadhaa, tatu kuu tatu ni hizi.

Mosi, ukisaga mahindi au nafaka zingine bila ya kukoboa unapata unga mwingi kwa kila kilo utakayoisaga.

Hivyo ifahamike kuwa kukoboa kunapoteza kiasi fulani cha unga. Pili, unga usiokobolewa una kiasi kikubwa cha mafuta, protini, madini, vitamini, na nyuzinyuzi (fibre). Kwahiyo, unaimarisha zaidi lishe ya mlaji. Kama watu watajenga tabia ya kula mahindi ya kuchoma, kuchemsha au kupika kande pia wanapata faida kubwa ikiwemo kupata choo kikubwa mara kwa mara.
Tatu, kuandaa unga usiokobolewa na kazi rahisi katika ngazi ya familia. Nne, mara nyingi unga usiokobolewa bei yake ni nafuu.

Faida ya unga ulikobolewa

Unga uliokobolewa nao unafaida zake kadhaa. Unga uliokobolewa unapendwa na watu wengi kutokana na kuwa na radha nzuri na rangi ya kuvutia.

Kwahiyo, mtu anaweza kula ugali wa kutosha na kupata nishati inayohitajika na mwili wake.

Unga uliokobolewa unaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu bila kuharibika kwa sababu ya kuwa na kiasi kidogo cha mafuta.

Unga uliokobolewa ni rahisi kuupika. Pumba zinazotokana na kukoboa nafaka zinaweza kutumika kwa kulisha mifugo, kuzalisha nishati, kutengeneza mbolea na matumizi mengine.

Madini ya chuma na zinc yaliyomo kwa wingi katika nafaka mbambali yanaweza kutumika kwa kiwango kikubwa na mwili kama mtu atakula chakula kilichopikwa kutokana na unga uliokobolewa.

Hii ni kwa sababu nafaka zina kemikali inayoitwa "phytate" ambayo inauzuwia mwili kunyonya madini hizo na kutumika mwilini. Ukikoboa nafaka kama vile mahindi unapunguza kiasikibwa cha kemikali hiyo ya "phytate".

Faida na hasara

Kwa maelezo ya hapo, ni dhahiri kuwa kukoboa nafaka kuna faida na hasara zake. Tumeona kuwa ukikoboa nafaka kama vile mahindi unapoteza baadhi ya virutubisho kama vitamin, madini na nyuzi nyuzi.

Inashauriwa kwa mtu anaekula chakula kilichopikwa kutokana na unga uliokobolewa ale na matunda na mboga za majani za kutosha ili kuziba pengo la vitutubisho vilivyopotea wakati wa kukoboa.Kwa mtu anaweza kutumia unga usiokobolewa (dona) ni muhimu kwake kufanya hivyo kwa sababu faida zake ni nyingi.
Akumbuke kuwa asage kiasi kidogo au anunue kiasi kidogo cha dona ili usiharibika kutokana na kukaa sana kabla ya kupikwa.

Kwa upande wa mchele, watu wanashauriwa wasiuoshe sana wakati wanataka kuupika.VYAKULA NA MAGONJWA; Faida na hasara ya unga wa mahindi wa kukoboa - mwanzo - mwananchi.co.tz







 
Nyumbani kwangu nilishapiga marufuku kula ugali uliotokana na unga uliokobolewa.
Sembe ni chanzo kikubwa cha ugumu wa kupata choo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…