Vyakula sokoni bei iko chini sana

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Leonilienda siko la Buguruni nilichokutana nacho. Nyanya kisado 2500

Nyanyachungu fungu la 2000 hubebi. Viazi mviringo kindoo kidogo 3000

Mchele 1800. Vitunguu vya 2000 huwezi kubeba

Dkt. Mwigulu au marehemu Mafuru mlifanyafanyaje hapo?

Au ndio kuadimika kwa shilingi.
 
Cha ajabu huku mikoani hali ni tete.

Ukishjndwa kuishi Dar hakuna mahali.utaweza.
 
Niliambiwa na mzee mmoja kiwa soko la Buguruni na temeke ndio masoko yenye bidhaa zenye bei ndogo zaidi kwa Dar nzima,hii ni kutokana na jamii iliyomzunguka masoko hayo ni ya kimaskini hata karoti na hoho wanauza hadi nusu kwa hamsini

USSR
 
Uko sahihi,soko la temeke ndio funga kazi,vitu bei chee sana
 
Buguruni mbona kawaida vitu kuwa cheap?
 
Binadamu hawana wema. Vyakula vikipanda tunapiga kelele, serikali haikemei wafanyabiashara wwnapandisha bei ziko juu. Leo vyakula bei iko chini mnalalamika. Ndiyo maana Magufuli aliwaambia wakulima uzeni mahindi hata laki 5 gunia, maana hawakukusaidia kulima. Vyakula bei au kushika huamuliwa na nguvu ya soko lenyewe. Mwaka jana alizeti ilikuwa 50,000 kwa gunia leo hii ni 130,000.
 
Supply na Demand...

Mbona mambo ya kawaida sana haya..

Msimu wa mvua si umeanza?

January nenda kaulizie bei za nyanya na vitunguu uone kama haujakimbia..

Vitunguu kuna msimu vinafika hadi 5,000/= kwa kilo moja. Na kuna msimu kilo moja inauzwa mia tano (500/=).
 
Uko sahihi,soko la temeke ndio funga kazi,vitu bei chee sana

Nchi zenye uchumi wa kujikimu kama tanzania hiyo kawaida.. sababu mazao na vyakula vinazalishwa kufuata misimu sababu asili
Kuwa wakulima wetu Kilimo chai ni cha kijima cha kufata msimu na asilimia kubwa hao wakulima wanategemea soko la ndani .. matokeo yake vyakula
Vinajazana sokoni.. na ukichukia jamii ya matunda na mbogamboga vinawahi kuharibika inabidi wakulima wauze kwa bei chee walau warudishe mtaji..

Kila mwaka unakuta msimu wa nyanya zinashuka sana bei same goes to matunda kama machungwa.. baada ya mwez au miezi miwili utakuta nyanya moja shilngi 300..

Kwasababu hatuna vuwanda vya kutosha vya kusindika vyakula na pia serikali hiweki bidii ya ku lobby huko nje kupata masoko ya nje kwa Wakulima wake.. ndo maana kutoboa katika l kilimo.. ni kazi sana..
 
Niliambiwa na mzee mmoja kiwa soko la Buguruni na temeke ndio masoko yenye bidhaa zenye bei ndogo zaidi kwa Dar nzima,hii ni kutokana na jamii iliyomzunguka masoko hayo ni ya kimaskini hata karoti na hoho wanauza hadi nusu kwa hamsini

USSR
Buguruni inauzwa mpaka hoho nusu, yaani unaenda unakatiwa hoho nusu unaenda kuunga mboga
 
Kwa hyo unataka wauze bei kubwa bidhaa zao zioze!?😂
 
K
Wapi kalalamika????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…