Vyakula vilivyounguwa (chips) vinasababisha Kansa

Vyakula vilivyounguwa (chips) vinasababisha Kansa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
1185175_212833342216144_1622980353_n.jpg


VYAKULA VILIVYOUNGUWA (CHIPS) VINASABABISHA UGONJWA WA


KENSA TUJIHADHARI SANA KULA HIVYO VYAKULA.


Wanasayansi wanasema kuwa wanawake ambao hula chips au 'crips' kila siku wanaweza kuongeza mara mbili hatari ya kensa ya kizazi na ya ovari.


Hatari hiyo inatokana na mada iitwayo acrylamide, ambayo hupatikana wakati wa kukaanga, kuoka au kuchoma vyakula mbalimbali. Wataalamu


wa Kidachi wamewafanyia uchunguzi watu 120,000 juu ya tabia yao ya ulaji na kugundua kuwa wanawake ambao wanakula vyakula vyenye


acrylamide, wanaonekana kukabiliwa na hatari zaidi ya kupatwa na aina hizo za saratani. Vyakula ambavyo vinapata rangi mbalimbali au kuungua


wakati wa kupikwa vinaonekana kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na acrylamide. Wataalamu wa vyakula wanasema kuwa, ni wazi kuwa


haiwezekani kuondoa aina hizo za vyakula moja kwa moja katika lishe yetu. Uchunguzi kuhusiana na masuala hayo umeonyesha kuwa, wale ambao wanakula mikrogram 40 za acrylamide kwa siku ambayo ni sawa na nusu


ya pakiti ya biskuti, sahani ya chipsi ya paketi moja ya crisp, basi wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na kensa mara mbili zaidi ikilinganishwa


na wale wanaokula acrylamide kwa kiasi kidogo zaidi ya hicho. Hata hivyo wataalamu wa uchunguzi huo wanawatoa shaka watu kwa kusema kuwa, matokeo ya uchunguzi huo yanapaswa kuthibitishwa zaidi na uchunguzi mwingine.
 

Attachments

  • Burger king.jpg
    Burger king.jpg
    127.3 KB · Views: 138
  • dangers-of-eting-junk-foods.jpg
    dangers-of-eting-junk-foods.jpg
    34.2 KB · Views: 135
  • nyama choma.jpg
    nyama choma.jpg
    22.5 KB · Views: 163
  • Piza huts.jpg
    Piza huts.jpg
    11 KB · Views: 126
  • pweza.jpg
    pweza.jpg
    12.2 KB · Views: 127
  • junkfood.jpg
    junkfood.jpg
    27.6 KB · Views: 126
Back
Top Bottom