Vyakula vya siku hizi havina harufu kabisa

Wapishi wa siku hizi nao wavivu pia inachangia viungo wananunua vishasagwa au kumenya unategemea harufu itatokea wapi? Kitunguu thomu kinamenywa mwezi mzima kinatiwa kwa plastic alafu upishi wenyewe pia tunaripua hatuna tungo Kama wazee wetu wa zamani kwa mfano mchuzi ulikua unapikiwa kwenye chungu cha udongo siku hizi kwenye sufuria wengine hata kwenye microwave N.k
 
Ukipata ndugu/jamaa anayetokea maeneo unakolimwa mpunga agiza kitu cha asili, ukitegemea kununua mtaani utaishia Kula products za Thailand, kupata radha mpaka ujaze maviungo kibao kwa dinning table
 
Ukipata ndugu/jamaa anayetokea maeneo unakolimwa mpunga agiza kitu cha asili, ukitegemea kununua mtaani utaishia Kula products za Thailand, kupata radha mpaka ujaze maviungo kibao kwa dinning table
Ni kweli mkuu,vyakula vya siku hizi ni shida.Hadi kuku wa kienyeji kakosa ladha,nilipouliza kulikoni... ninaambiwa na wenyewe wanapewa vyakula vya kisasa.
 
Nahisi matumizi ya madawa ya kuulia wa dudu na matumizi ya mbolea za viwandani mashambani yamechangia sana kuharibu harufu nzuri ya vyakula zamani samadi ilitumika
 
Mbona mnaenda mbali nyama tu za ng'ombe za siku hizi hazina ladha kama za zamani au kwa vile wa dar kwenye vyakula hasa mchele enzi za mwalimu kuna mchele mmoja matata sana mchele wa mbeya walahi ulikuwa ukiuweka kwenye kabati la vyakula au kwenye ndoo ukiufunua mwaaa harufu nzuuuri unahisi kula bila kupikwa siku hizi mmhh majanga ule udongo wa zamani uliokuwa na rutuba ya asili tumeuharibu na kilimo sasa amini hivyo hawa wazungu wana lao jambo hata enzi ya mwalimu ulikiwa ukienda vijijini utakutana na kila aina ya matunda siku hizi mmh hata ile miti yenyewe inazidi kupungua.
Ukweli .....zamani pilau inanukia mtaa mzima
siku hizi pilau hata nyumba kumi ikipikwa husikii
 
Mikate ya siku hizi hayaoti ukungu(mold) pamoja na kuhifadhiwa muda mrefu. Je nini madhara ya preservatives zinazotimika kwa afya zetu?
Sema la ukweli nimezunguka maeneo mengi sio kama nafagilia sijawahi oma mikate mitamu kama mikate fulani hivi inatengenezwa Arusha kweli huishi kuila kuna mingine ya njano uupate wa moto moto na ile meupe weka mbali na watoto hii huku najionea ipo ipo tu
 
....labda unakula vya mchina Mkuu.

 
Zamani ukipikwa wali maharage,yaani lazima sinia iwe nyeupe,

siku hizi vijiko vitano sahani unasukuma kule.

Vyakula vimego evolution labda,
 
Mkuu unazungumzia mikate ya Super loaf au
 
Hahaa umenikumbusha mchuzi au mboga za majani upikie kwenye chungu na jiko la mkaa au kuni weee sio kujilamba huko
 
Mkuu unazungumzia mikate ya Super loaf au
Sijui inaitwaje lakini ni mikuubwa kwa juu imefungwa na kama kaplasiki kaguumu aa hii mikate poa sana sijawahi ona huku dar sijawai ona mikate mingi wanalipua lipua
 
Sijui inaitwaje lakini ni mikuubwa kwa juu imefungwa na kama kaplasiki kaguumu aa hii mikate poa sana sijawahi ona huku dar sijawai ona mikate mingi wanalipua lipua
Super loaf mikate mitam sana asee.
 
... Umenikumbusha zamani ile mikate ya Siha, yaani hata gani halijaishusha dukani unasikia harufu yake nzuri...
 
Tatizo ni maji, maji ya sasa yana kemikali nyingi sana zinaa harufu
 
Pole kwa yaliyo kukuta naona ni kwako tu ndugu yangu
 
Weee mleta mada uko sahihi. Nakumbuka kipindi hicho sichezi mbali na home. Wali unapigwa bila mboga, lakini unashuka kooni kwa speed ya light (3x10E8 m/s)
 
Tuliacha kulima vyakula vya asili yetu kisa mabadiliko ya tabia nchi sasa tunakula vyakula ambavyo mbegu zake nimefanyiwa michakato kwenye maabara kama seedco na watafiti wengineo. Zamani ilikuwa ukila hindi la kuchoma lilikuwa tamu sana haya ya siku hizi hata ukilitoa shambani muda huo huo na kulichoma bado radha yake kawaida sana
 
Kuna mchafuko wa hewa!! Inakua ngumu harufu nzuri kupenya. [emoji23][emoji23]
 
Vyakula vingi vya dar havina ladha ila ukiwa mkoani vikapikwa fresh vina taste aisee. Pia sikuhizi kuna michakachuo ya misosi. Wali uwe mtamu upikwe na mkaa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Una utani na watu wa Dar eeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…