Vyama hivi vya siasa lazima viathirike, kama rasimu hii itapita.

Vyama hivi vya siasa lazima viathirike, kama rasimu hii itapita.

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,149
Reaction score
3,825
Rasimu ya katiba imeweka 'vizingiti' kwa watakao gombea nafasi fulani fulani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Vizingiti hivyo ni 'elimu' na 'umri', hii inatokana na umuhimu wa elimu katika kuendesha shughuli mbalimbali za mwanaadamu kwa usahihi na umakini.

CHADEMA kama mdau wa siasa nchini, ni chama kitakacho athirika vibaya na kigezo cha elimu kupewa kipaumbele.

Hii ina sababishwa na viongozi wengi wa chama hichi kuongoza kwa mazoea (uongozi ni kipaji) wakati siasa ya sasa inapaswa ifanywe kitaalamu.

Maeneo ambayo CHADEMA itaathirika sana katika uchaguzi mkuu ujao ni ya 'URAIS' na 'UBUNGE', kufuatia kiwango kipya cha elimu kuwekwa kama kigezo cha mtu kupata uhalali wa kugombea.

Kwa upande wa urais, mgombea anapaswa awe na angalau shahada, aidha kwa upande wa ubunge mgombea anapaswa angalau awe na elimu ya kidato cha nne. Kwa viwango hivi vipya, 'majembe' ya CHADEMA hayata wania nafasi tajwa.

Kwa rasimu hii, upinzani umeathiriwa zaidi, kwani elimu ndio kitanzi chetu CCM dhidi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini.

Asante jaji Warioba, asante Tume.
 
yaani wewe mvivu kufikiri pale cdm mimi mwanachama tu ni degree yangy safi kwaiyo nkigombea je itabadilika na kuwa la saba kama maji marefu eeeh. hakuna chama chenye wasomi wenye uwezo kama chadema
 
Mimi nilipendekeza viwango vya chini vya elimu viwe, rais iwe ni Master na ubunge iwe Degree, udiwani form six na wengine wote wawe form four.
 
Mkuu, ningekuona wewe kuwa ni GT wa JF iwapo uzi wako ungeambatana na mifano halisi ya "wabunge na wagombea urais wa kudumu" wa hicho chama CHADEMA waliopo. Weka mkazo katika "wa kudumu". Hapo ndipo mantiki ilipo.
 
yaani wewe mvivu kufikiri pale cdm mimi mwanachama tu ni degree yangy safi kwaiyo nkigombea je itabadilika na kuwa la saba kama maji marefu eeeh. hakuna chama chenye wasomi wenye uwezo kama chadema

Mkuu, wewe kwani ni 'jembe' CHADEMA? maana kwenye maelezo yangu nimesema 'majembe' ya CHADEMA hayata pata fursa ya kugombea, na ni imani yangu unawajua hao majembe yenu huko CHADEMA.
 
Mimi nilipendekeza viwango vya chini vya elimu viwe, rais iwe ni Master na ubunge iwe Degree, udiwani form six na wengine wote wawe form four.

Sasa kama mapendekezo yako yangechukuliwa huoni kama CHADEMA ingefutwa kabisa? maana majembe yake yote yana vi-diploma vya kuunga unga tu.
 
Rais angefikia ngazi ya PhD labda maana tunadhani uongozi ni kuwa na elimu kubwa,
 
Back
Top Bottom