Nguvu kubwa (wakati mwingine isiyokuwa na sababu) inatumika na vyama shindani kuwaaminisha wapiga kura kuwa wao ni bora zaidi.
Walisema wahenga kizuri chajiuza. Nasi wapiga kura macho tunayo.
Enyi vyama na hata wagombea hebu msitulazimishe wala kutufokea.
Kwa hakika, kila mmoja wenu na ajiandae kisaikolojia kukubali kushindwa katika zoezi litakalokuwa huru na la haki.
Enyi tume na mamlaka zote waacheni mafahali hawa waumane waamuzi wakiwa ni sisi. Kwenu nyie ni kutupa zoezi litakalokuwa huru na la haki katika namna ambayo washindani wote nasi wapiga kura tutaridhika.
Tunataka uchaguzi ulio huru na wa haki ambapo watakaoshindwa, bila ya kinyongo watapiga simu kumpongeza mshindi.
Uchaguzi huu usitupeleke kubaya. Tusimwachie mola peke yake, amani ni tunda la haki!
Kujipanga kufanikisha zoezi la haki inawezekana.