Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Vyama vya kufa na kuzikana havina tija kwa muhusika anayechangia, kwa sababu atasubiriwa afe yeye au ndugu na jamaa ndipo chama kianze mchakato wa kumzika.
Nilikuwa nashauri, kwa nini hivi vyama visisomeke, Kuuguzana na kuzikana? Ikiwa na maana ya kupigania uhai wa mwanachama, ambapo ndio sehemu muhimu zaidi katika maisha yake; kuliko kusubiria mpaka umauti umfike ndipo waanze mchakato wa mazishi.
Kwa mtazamo wangu, kama hivi vyama vitaendelea kujikita kwenye kufa na kuzikana, naona havina maana yoyote kwa muhusika, zaidi tu ya maonyesho.
Kwa sababu sehemu ngumu ya maisha ya mwanadamu huwa ni kwenye kupigania uhai wake; kuhusu maziko hakuna shida, ata akizikwa na mtu mmoja hakuna baya.
Kwa upande wenu mna maoni gani?