Pre GE2025 Vyama vya siasa vinavyojipiga kifua mitandaoni huwa vinaumbuka sana wakienda kuonana na wananchi ana kwa ana

Pre GE2025 Vyama vya siasa vinavyojipiga kifua mitandaoni huwa vinaumbuka sana wakienda kuonana na wananchi ana kwa ana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Huwa vina kutana na hali ya kushangaza sana, ngumu na tofauti kabisa na majivuno, majigambo na ujasiri wa mitandaoni..

Field huwa vinakuwa vidogo zaidi ya piritoni, dhaifu sana, vimenyong'onyea mno, havina watu wala hamasa hata kidogo. Wao hushangaa wananchi na wananchi huwashangaa wao, nanajikuta wanashangaana🤣

Vinajikuta havifahamiki wala wagombeaji wao hawajulikani, wala kueleweka na wananchi wa eneo husika! Sera, mipango na mikakati yao ndio kabisa huwa ni tofauti na mahitaji halisi ya wananchi.

Hali hiyo huwapa mihemko na ghadhabu sana, saa zingine mpaka kufikia hatua ya kudhihaki wananchi wapiga kura kwa maneno ambayo mpaka leo yanatesa baadhi ya vyama vya siasa mpaka leo. Dharau na kebehi za kujipa umuhimu zaidi ya wengine kwa dhihaka ni kitu mbaya sana aise.

Zaidi sana, vyama vya mitandaoni, hata ofisi huwa havina huko field na hivyo kupoteza imani na matumaini kabisa kwa wananchi wapiga kura, kwamba wagombeaji wa vyama hivyo ni wapiga dili tu, yaani hata ofisi ya kufanyia kazi zao za kichama hawana, halafu wapewe dhamana ya uongozi?

Wananchi hujawa hofu kwamba viongozi hao wasiojulikana na wasio na ofisi, kwamba wakipotea au kukimbia na dhamana za wananchi wanazo zisimamia kwa niaba, watapatikana wapi?
 
Back
Top Bottom