Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Baada ya kuona mchakato wa ndani wa vyama vya siasa kupata wawakilishi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nimeona nije na ushauri huu hasa baada ya kuona watia nia wengi wakiwa wanaume, hadi wengine kupelekea kujinadi kama wanawake.
Kuwapa nafasi za upendeleo na kipaumbele wanawake wagombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 ni hatua muhimu kwa vyama vya siasa inayoweza kukuza mabadiliko ya kijamii na kisiasa. Chaguzi zilizopita tumeshuhudia ushiriki usioridhisha wa wanawake kutokana na sababu mbalimbali. Ifike wakati wanawake waaminiwe kuongoza wananchi kuanzia huku kwenye ngazi za chini ili waweze kuchochea mabadailiko
Itasaidia kupunguza pengo la uwakilishi wa kijinsia kwenye nafasi za uongozi na kufanya maamuzi. Uwiano wa kijinsia unaochagizwa unatoa nafasi ya kuwasilisha maslahi, changamoto, na sauti za wanawake, watoto, wazee katika mchakato wa maendeleo ya jamii.
Kuwapa fursa wanawake wenye uwezo wa uongozi: Ingawa kuna wanawake wengi wenye uwezo wa kuongoza, wengi wao wanakosa nafasi kutokana na changamoto za kijamii, kiuchumi nk. Upendeleo wa kipaumbele kwa wagombea wanawake husaidia kuondoa vikwazo hivyo na kutoa jukwaa la kufikia malengo yao ya kisiasa na kijamii.
Tumeona viongozi wengi wa ngazi za Juu ambao wamekuwa role model wa wasichana wengi wenye ndoto, Mathalani Rais Samia, ambaye amefungua njia kuonesha kuwa Wanawake wanaweza. Hivyo wakiwa viongozi wa Mitaa wanakuwa mfano bora kwa wasichana na wanawake vijana, wakionesha kuwa uongozi na nafasi za kufanya maamuzi ziko wazi kwa jinsia zote. Hii huchochea wanawake wengi zaidi kujiamini na kujitokeza kushiriki kwenye nyanja mbalimbali za maisha.
Ni hayo tu wakuu, wanawake tuwaamini na wawezeshwe ili waweze kugombea, hivi juzi nimemsikia mbaba wa CCM akishawishi wanawake wampigie kura kwasababu yeye pia ni mwanamke mwenzao, hii ni ishara kuwa hata wanaume pia tunatambua nguvu waliyonayo wanawake katika uongozi.