Elections 2010 Vyama Vya Upinzani Iringa Mjini Vyaungana: V.O.A

Elections 2010 Vyama Vya Upinzani Iringa Mjini Vyaungana: V.O.A

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
10,827
Reaction score
4,176
Voice of America (Idhaa ya Kiswahili) inaripoti kuwa vyama vya upinzani 14 katika jimbo la Iringa mjini vimeungana kukabiliana na Gwiji Chadema na Mafisadi CCM.

Kwa mujibu wa habari hiyo, Chadema hawamo katika ndoa hiyo haramu wakirejea taarifa za kikachero kuwa huo ni mpango mzima wa Chama Cha Mafisadi (CCM) kupunguza kura za Chadema.

(Hii hapa ni kwa Wana-iringa tu. Siyo kwa Wana-JF).

Waacheni wagombea waungane na unafiki wao.Walisha Chukua Chao Mapema hao. Si munajua Bilal amerudi tena huko (munafiukiri amefuata nini kama siyo kufungisha ndoa haramu?) Kwenye masanduku msitende dhambi ya mkamkosea Mungu.Chagueni Chadema.
 
Watapata kama kura 50 hivi au less? Ukitaka kujua ni mpango wa nani angalia habari ilvyoshabikiwa kwa picha katika gazeti la HabariLeo na Daily News online huku msisitizo ikiwa ni kuwa ISIPOKUWA CHADEMA. Haishangazi pia vyombo vya habari vimekuwa vikijaribu kuinua CUF hoping watapunguza kura za CHADEMA. I can feel for them! PEOPLES POWER
 
Chadema hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Muungano wa viwete votes NCCR 6 CUF 13 TLP 4 UDP 1 SAU 0 UPDP 0 NRA 0 total = 24.
 
na bado mwaka huu watakoma, kwani ni mwaka wa mabadiliko.
 
Hivyo vyama vilivyoungana, muungano uko tangu mwanzo wa kampeni. Mahudhurio ya wananchi kwenye kampeni za huo Muungano ni hafifu sana, sina hakika kama CCM ina mkono kwenye huo Muungano. Japo kwenye kampeni zao wamekuwa wakimshambulia sana Mchungaji Msigwa kwa kumwaga matusi kiasi kwamba kuna mpiga debe wao mmoja ilibidi apewe onyo kali kwa kutumia lugha kali na chafu dhidi ya mgombea wa CHADEMA.

All in all, huo Muungano hauna nguvu.
 
Pombe ile ile, walevi wale wale na mabaa medi pia wale wale. House of Great Thinkers indeed. :becky: :becky: :becky:
 
Kama kuna mahali sisi m wanakosea ni katika eneo hili maana wao hupunguza kura zao. Ninao mfano halisi wa jimbo la Bukoba mjini.

Kuna habari za uhakika kuwa Hamis Sued Kagasheki alim-recruit jamaa aje kugombea kwa tiketi ya CUF ili kudhoofisha Chadema na kufanya mgawanyiko wa kura. Kwa wasiojua zamani Chadema haikuwa na nguvu sana bali CUF kwa kuwa watu wengi walikuwa wakimfuata kiongozi wao Wilfred Lwakatare wakati huo akiwa makamu katibu mkuu taifa CUF. Lakini huyu bwana alipoamua kujitoa CUF na kwenda Chadema aliondoka na kundi lote la watu. Kwa mahesabu ya Hamis alihisi anaweza kuweka mapandikizi kwa faida yake.

Lakini kwa uelewa wangu wa kisayansi nimegundua kuwa alifanya jambo jema maana kajipunguzia kura mwenyewe. Nasema hivi kwa kuwa najua wana Chadema ambao ni wengi sana katika jimbo la Bukoba hawawezi kwa namna yoyote kumpigia kura mwakilishi wa CUF. Na wana CUF ambao wapo na tena ni kikundi kidogo sana cha wana dini fulani, hawawezi kumpigia kura mwakilishi wa Chadema hata iweje. Lakini suppose kama kungelikuwa na wagombea wawili tu yaani wa sisi m na Chadema kwa vyovyote wale walio upande wa CUF wasingekuwa na jinsi na kwa vyovyote vile wangempigia kura wa sisi m ili kumkomoa wa Chadema. Na hapa ndipo hesabu zilipompiga chenga kagasheki. Namshukuru kwa kujipunguzia kura.

Wacha waungane hao mamluki waliojaa husuda tu ya mafanikio ya Chadema na kushindwa watashindwa maana hawana soko tena.
 
Tehe kama nawaona wanyalukolo wanapigwa na mtogwa(Ulanzi) wa mia tano tuu wanakunywaaaaaaaaaaaaaaaaaa wakiamka na hangover wananyosha vidole viwili CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAa
 
VYAMA 14 IRINGA VYAUNGANISHA NGUVU KUIBANA CCM NA CHADEMA
Mgombea wa umoja wa vyama 14 za upinzani jimbo la Iringa mjini Mariam Mwakingwe
Hizi ni baadhi ya Bendera za vyama hivyo vilivyoungana jimbo la Iringa mjini isipo kuwa Chadema
Mgombea urais wa APPT-Maendeleo Bw.Peter Mziray (kulia) akimnadi mgombea wa muungano wa vyama 14 jimbo la Iringa mjini Bi.Mariam Mwakingwe

Barua ya umoja wa vyama vya upinzani vilivyoungana jimbo la Iringa mjini
Monica Mbega (CCM)
Mchungaji Peter Msigwa (Chadema)
Aliyekuwa mgombea ubunge wa chama cha wananchi (CUF) Zaitun Mwaibula amejiunga na umoja wa vyama 13 za upinzani jimbo la Iringa mjini na kuongeza nguvu ya upinzani katika jimbo hilo hivyo kufanya jimbo hilo hadi sasa kubaki wa wagombea watatu wa nafasi za ubunge .

Wagombea wanaogombea katika jimbo hilo ni Monica Mbega (CCM) ,Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) na yule wa muungano wa vyama vya upinzani Mariam Mwakingwe (NCCR- Maguzi)

Vyama vinavyo muunga mkono Mwakingwe ni NCCR- MAGEUZI ,TLP, TADEA, SAU, CHAUSTA, APPT-MAENDELEO, JAHAZI ASILIA , CUF, NLD, UDP, MAKINI,DP, AFP NA UPDP.

Awali mgombea huyo wa CUF pamoja na kujaza fomu ya kuwania ubunge aliwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa Chadema mchungaji Msigwa baada ya kushindwa kutimiza masharti ya udhamini katika fomu yake.
source:Francis Godwin ni Iringa na matukio
 
mzimu wa mwakalebela unazidi kufukuta iringa?!!
 
Kifo cha nyaaaaaani............
Mwaka huu mafisadi imekula kwao!
 
Vipi kuhusu gharama za kampeni wanasaidiana au inakuwaje?? Mdau mwenye taarifa zaidi atufahamishe.
Ninashwaishika kuamini kuwa huu muungano si mtakatifu, maana kama ni kuungana wangeanza na wagombea wao wa urais
 
hawa ndio chadema hata kuwa pamoja na wenzao wanawafitini, kwa vp tuwape nchi hii?


CCM daima
 
Muungano wa viwete votes NCCR 6 CUF 13 TLP 4 UDP 1 SAU 0 UPDP 0 NRA 0 total = 24.
This word is offensive and should be edited either voluntarily or forcefully... Hata viwete ni watu

Unyanyapaa unaanzia kila sehemu, we should treat each one of us with the same respect, standard and dignity.... hujafa hujaumbika mkuu
 
Kuna habari za uhakika kuwa Hamis Sued Kagasheki alim-recruit jamaa aje kugombea kwa tiketi ya CUF ili kudhoofisha Chadema na kufanya mgawanyiko wa kura. Kwa wasiojua zamani Chadema haikuwa na nguvu sana bali CUF kwa kuwa watu wengi walikuwa wakimfuata kiongozi wao Wilfred Lwakatare wakati huo akiwa makamu katibu mkuu taifa CUF. Lakini huyu bwana alipoamua kujitoa CUF na kwenda Chadema aliondoka na kundi lote la watu. Kwa mahesabu ya Hamis alihisi anaweza kuweka mapandikizi kwa faida yake.

Kuwa mkweli kidogo na pia uelezee vipi huyo bwana alijitoa. Unaelekea utafikiri huyo bwana alijitoa wakati bado akiwa "makamu katibu mkuu taifa CUF" wakati ukweli ni kuwa alivuliwa hiyo nyadhifa kabla hajatimkia huko Chadema.

Kama washabiki wa CUF ni wale watu wa dini "flani", basi dini flani nyingine ndiyo watakuwa mashabiki wa Chadema? Au ukweli ni one sided tu? :becky: :becky: :becky:

Tungojee baada ya Oktoba 31 halafu hizi analysis zenu za "kisayansi" ndipo tutakapozichambua vizuri. :becky:
 
Kusema kweli hakuna uchaguzi ambao CCM inaonyesha kuogopa kama uchaguzi huu -- kuliko hata ule wa 1995 wakati wa moto wa NCCR. Kweli CCM maji shingoni, au puani tuseme!!!!
 
This word is offensive and should be edited either voluntarily or forcefully... Hata viwete ni watu

Unyanyapaa unaanzia kila sehemu, we should treat each one of us with the same respect, standard and dignity.... hujafa hujaumbika mkuu

Human Error. Msamehe bure. (Hata mimi nimemsamehe). Mod fanya kazi yako. use "Find and Replace"

Sidhani kama Mwana-Jamvi alikuwa akimaanisha kudhalilisha jamii ya wenzetu viwete.
 
Walie tu, mwaka huu hatudanganyiki, muungano hewa huo, sisi tunasonga. Lakini jamani mimi upinzani wa bongo nashindwa kabisa kuwaelewa, hivi kwa nini wana chuki hivi?? Kwa nini wasiunganishe nguvu pamoja na chadema ili waiondoe ccm? Ni wanamapinduzi wa kweli hawa au mapandikizi ya ccm???
 
Kura nyingine hizooooo kwa CHADEMA, pipoooooooooooooooooooooooooz, pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Back
Top Bottom