VYAMA 14 IRINGA VYAUNGANISHA NGUVU KUIBANA CCM NA CHADEMA
Mgombea wa umoja wa vyama 14 za upinzani jimbo la Iringa mjini Mariam Mwakingwe
Hizi ni baadhi ya Bendera za vyama hivyo vilivyoungana jimbo la Iringa mjini isipo kuwa Chadema
Mgombea urais wa APPT-Maendeleo Bw.Peter Mziray (kulia) akimnadi mgombea wa muungano wa vyama 14 jimbo la Iringa mjini Bi.Mariam Mwakingwe
Barua ya umoja wa vyama vya upinzani vilivyoungana jimbo la Iringa mjini
Monica Mbega (CCM)
Mchungaji Peter Msigwa (Chadema)
Aliyekuwa mgombea ubunge wa chama cha wananchi (CUF) Zaitun Mwaibula amejiunga na umoja wa vyama 13 za upinzani jimbo la Iringa mjini na kuongeza nguvu ya upinzani katika jimbo hilo hivyo kufanya jimbo hilo hadi sasa kubaki wa wagombea watatu wa nafasi za ubunge .
Wagombea wanaogombea katika jimbo hilo ni Monica Mbega (CCM) ,Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) na yule wa muungano wa vyama vya upinzani Mariam Mwakingwe (NCCR- Maguzi)
Vyama vinavyo muunga mkono Mwakingwe ni NCCR- MAGEUZI ,TLP, TADEA, SAU, CHAUSTA, APPT-MAENDELEO, JAHAZI ASILIA , CUF, NLD, UDP, MAKINI,DP, AFP NA UPDP.
Awali mgombea huyo wa CUF pamoja na kujaza fomu ya kuwania ubunge aliwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa Chadema mchungaji Msigwa baada ya kushindwa kutimiza masharti ya udhamini katika fomu yake.
source:Francis Godwin ni Iringa na matukio