Vyama vya upinzani nchini havishindwai uchaguzi kwa bahati mbaya tu

Vyama vya upinzani nchini havishindwai uchaguzi kwa bahati mbaya tu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Inasikitisha sana kuwa CCM na Tanzania tulitumia rasilimali nyingi sana ikiwemo kumwaga damu za watu wetu ili kuhakikisha kuwa nchi za kusini mwa Afrika zinaondokana na dhuluma za nyakati za uchaguzi zilizokuwa zikifanywa na wakoloni na makaburu ili vyama vya siasa vya wananchi visishiriki uchaguzi au hata vikishirki visishinde uchaguzi. Afrika Kusini ilikuwa huru lakini demokrasia kulikuwa hakuna, Pamoja ANC kuwa na wafuasi wengi lakini utawala ulikuwa wa chama cha makaburu tu walio wachache.

CCM imekopi na kupesti mbinu hizohizo za wakoloni na makaburu katika kuhakikisha kuwa inabaki madarakani litoke jua au inyeshe mvua. Kuna uwezekano mkubwa kuwa mbinu nyingine ambazo Mzee Mwinyi hakuzitaja ni CCM kuunda vyama bandia vya siasa vinavyoiunga mkono CCM au kupandikiza makada wa CCM kwenye vyama vya upinzani.



Uchanga wa vyama kushindwa kushinda uchaguzi sio kweli, kule Israel mtu anaunda chama chake kipya miezi 2 kabla ya uchaguzi na kinashinda uchaguzi au kushiriki kuunda serikali.



Tumuunge kila mtu anaedai Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi inayokubalika kwa vyama vyote ili anaeshinda ashinde na anaeshindwa asubiri uchaguzi mwingine bila manung’uniko. Haiwezekani kuwa na tume ambayo inawezekana kabisa kuengua 100% ya wagombea wa uchaguzi wa vyama vingine na kubakiza 100% ya wagombea wa CCM. Hata kama unataka kusita kukubali madai ya kuwa tume sio huru inakuwia vigumu kuyakataa madai hayo. Hata makaburu hawajawahi kufanya hivyo
 
Point iwe katiba mpya kwa maslahi mapana ya taifa,sio katiba mpya ili vyama pinzani vishinde chaguzi.
Isionekane mahitaji ya katiba mpya ni kwa maslahi ya kisiasa tu bali katiba itakayokuja kutatua changamoto zetu za muda mrefu kama nchi.
 
Point iwe katiba mpya kwa maslahi mapana ya taifa,sio katiba mpya ili vyama pinzani vishinde chaguzi.
Isionekane mahitaji ya katiba mpya ni kwa maslahi ya kisiasa tu bali katiba itakayokuja kutatua changamoto zetu za muda mrefu kama nchi.
Maslahi mapana ya taifa yanaanzia kwenye uchaguzi mzuri ambao matokeo yake yanakubalika na watu wengi. Taifa linadumaa kama kuna watu wengi ambao hawaikubali serikali iliyoko madarakani kwasabu ya uchaguzi ulivyoendeshwa.
 
Back
Top Bottom