Tetesi: Vyama vya upinzani(Ukawa) kususia chaguzi zijazo.

Tetesi: Vyama vya upinzani(Ukawa) kususia chaguzi zijazo.

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalaam, Kuna taarifa zimevuja kwamba vyama vya upinzani nchini(ukawa) vimezamiria kutoshiriki chaguzi zote zitazoitishwa na tume ya uchaguzi (NEC) kwa madai kwamba hii tume ni mali ya Ccm na imesheheni makada wa ccm. Mmoja wa wenyeviti wa ukawa amesema wanajiandaa kutoa tamko la pamoja la kutoshiriki uchaguzi wowote utaoitishwa na tume hii ya leo kwani haiko huru na haiwezi kutenda haki, kwani ipo kwa maslahi ya ccm.

Nimetafakari nikajiuliza km hili litawekana maana viongozi wa upinzani wengi wananjaa na niwasaliti miongoni mwao, pia wengi ni mapandikizi ya ccm wapo upinzani ili kudhoofisha nguvu ya upinzani. Mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mitaa ngoja nivute subra nione km tetesi hizi zinaukweli.
 
Unatemba barabarani ukiongea peke yako!!
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa hautakiwi kususiwa mana viongozi wake ni watu wasio na maslahi zaidi ya kuwatumikia wananchi. Uchaguzi wa serikali za mitaa usipokua na matamshi ya hatari kama yale ya UVCCM kule Arusha ,utakua hauna tatizo lolote na utakua mzuri tu mana unafanywa maeneo ya watu wenyewe na wanahesabu wenyewe na wanajuana. Sehemu isiyo na chama Fulani inajulikana kabisa na anayelazimisha kushinda anapata shida sana kuongoza.

Nakumbuka enzi za Chama Kimoja watu walikua wanaombwa sana kugombea nafasi za serikali za mitaa na wengi walikua wanakataa.

Kwa sasa bado naamini watu wengi ni waadilifu na uongozi kwao ni mzigo mzito unaohitaji uadilifu na uzalendo wa Kweli.

Nafasi nyingine za Ubunge na udiwani watu wanatumia Nguvu kubwa kuhakikisha wanashinda hata kwa bao la mkono kwa sababu ya maslahi makibwa yanayopatikana huko na wengine kupata mpaka uwaziri.

Hakuna Uzalendo kwenye siasa inapotokea suala la madaraka mana watu wanachokitolea macho niaslahi yanayopatikana huko.

Kidogo Uzalendo nimeuona kwa Wazanzibar hasa wapinzani mana waliamua kuachia maslahi manono ya uwakilishi na umakamu wa kwanza wa Rais kwa sababu ya kutetea walichoamini.
Sio jambo dogo hilo ni kujitoa kweli kweli.

Tume kwa kweli na msajili wameamua kuua Demokrasia kwa kujionyesha wazi kuwa ni makada wa Chama cha mapinduzi .
Sio jambo zuri kwa watu wachache waliopewa dhamana kwa muda kuharibu mustakabali wa taifa letu ulioko kikatiba.

MUNGU tusaidie tuwapate wajumbe wa Tume waadilifu na wazalendo wa kweli sio wa kulinda Tumbo bali kulinda Katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom