Pre GE2025 Vyama vya upinzani vijijenge kitaasisi na sio kusubiri uchaguzi na kuanza kuleta malalamiko

Pre GE2025 Vyama vya upinzani vijijenge kitaasisi na sio kusubiri uchaguzi na kuanza kuleta malalamiko

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Feb 11, 2020
Posts
5
Reaction score
2
Kumekuwa na Sintofahamu kuhusu mchakato wa baadhi ya vyama vya siasa kupata wawakilishi kuelekea uchaguzi wa serekali kuu na uchaguzi wa mwakani.

Vyama vingi vya siasa vimekua vikilalamika wagombea wao kuenguliwa kwa kukosa sifa za kugombea kwenye Chaguzi hizo, japo madai haya bado hayajathibitika ila ukweli ni kwamba maandalizi duni, pamoja na uhafifu wa juhudi za kujijenga kitaasisi kumekua mwiba kwa baadhi ya vyama hivyo.

Mathalani mchakato wa kuwapata wagombea wao umekua n wa kustukiza hivyo kushindwa kupata wagombea wenye uzoefu na taratibu za uchaguzi pamoja na sheria na kanuni zake...

Katika hali ya tofaut chama tawala (CCM) kimejitanabaisha wazi kwa kuweka mfumo mkali na wa wazi wa kuwachuja watia nia katika nafasi mbalimbali za uongozi, hivyo kuwafanya wagombea wao kuwa na uzoefu na taratibu,sheria na kanuni za uchaguzi, michakato hii huanza mapema na kujenga uelewa mkubwa kwa wagombea.

Soma Pia:
Rai yangu kwa vyama vingine ni kuendelea kujiimarisha kitaasisi ili kuweza kuweka wagombea wenye uwezo na sio wa kushtukiza
 
Hahaha yani CCM/SERIKALI ndio unaita TAASISI? Katiba mpya iletwe, hivi vyeo vya kupewa KICHAWA viondoke, viombwe na wenyesifa wapewe uone kama CCM itabaki.

Sasa hivi CCM inateua kila nafasi serikalini, ndio maana unaoan UVCC na UWT wamejazana watu huko kungoja teuzi.
Weka Katiba mpya ni suluhu ya kilio chako, utajifunza nini maana ya Taasisi.
 
Vijijenge kivip maana wakiita mkutano polisi hawa hapa eakikaa kikao cha ndani polisi hawa hapa yaaan upinzani hapa tz wanaonekana km ni majambazi.Sasa wajijenge mda gani????Cha msingi ni vyama vya siasa waache ufala watakua mafala mpaka lini jino kwa jino ndo sulihisho.
 
Punguza unafiki. Vyama vya upinzani vipongezwe hasa CHADEMA maana vinafanya kazi katikati Mazingira magumu. Mfumo uliopo ni wa chama kimoja, ndio maana wakuu wa mikoa , Wilaya, wakurugenzi etc wanapambana na vyama vya upinzani kila kukicha bila kusahau polisi , Usalama wa Taifa na mahakama.

Kwa hivyo, punguza unafiki na ujinga kuangalia jambo kwa jicho la kulaumu baadala ya kuangalia mfumo ambao vya hivi vya upinzani vinafanya kazi.
 
Back
Top Bottom