Ragamuffin
Senior Member
- May 2, 2009
- 160
- 6
MENGI TO ACCOUNT FOR 'SILVERDALE FARM'
26.05.2009 1132 EAT
Serikali yabariki mkataba kuvunjwa26.05.2009 1132 EAT
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Na Nakajumo James,Moshi [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]SERIKALI imebariki maamuzi ya vyama vitatu vya ushirika vya msingi Uswa Mamba, Shari na Kyeri wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kutaka kuvunja mkataba na kampuni ya uwekezaji ya Fiona (T) LTD. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kilimanjaro, Kasya Kasya, aliyasema hayo wakati akizungumzia mgogoro baina ya mwekezaji huyo na bodi ya vyama hivyo. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Alisema mkutano wa vyama hivyo chini ya mwenyekiti wake, Bashiri Shoo, uliofanyika Mei 11 mwaka huu ulikuwa na baraka zake, baada ya yeye kuwa na majukumu mengine ya kiofisi. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Katika mkutano huo wanachama zaidi ya 300 vyama hivyo vilimtaka wakili wao, Apolo Maruma kumuandikia notisi ya siku 30 mwekezaji huyo, Fiona (T) Ltd, awe amekabidhi shamba kwa vyama hivyo. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Wanachama ndiyo wenye uamuzi wa mwisho na mali yao ambayo ni mashamba waliyomkabidhi mwekezaji, hatua ya kutaka kuvunja mktaba mimi siipingi, ila wafuate taratibu,alisema Kasya. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Aidha vyama hivyo viliazimia kutoutambua mkataba wa maridhiano na mwekezaji huyo ambao pamoja na mambo mengine unaeleza kumsamehe deni la Sh milioni 72. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Akizungumzia uamuzi wa vyama hivyo, Kasya alivitaka vyama hivyo kutumia utaratibu uliotumika kuingia mkataba huo ili kuweza kuuvunja kama walivyoazimia. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Alisema vyama hivyo vinamlalamikia mwekezaji huyo kwa madai kwamba baada ya kufanya vyema katika miaka ya 1999 hadi 2003 kwa kuendeleza zao la kahawa, baada ya hapo alianza kungoa kahawa na miti na kuotesha Mahindi na Maharage. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kwa upande wake, mwekezaji huyo, Benjamin Mengi, alipohojiwa kuhusu hali hiyo alishikilia msimamo wake kwamba hatambui maamuzi ya mkutano huo.[/FONT]
Last edited by a moderator: