Vyama vyakabidhi mapendekezo sheria ya katiba

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
[h=2][/h]


Na Muhibu Said



23rd October 2013














Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia


Hatimaye vyama vya siasa vilivyo na uwakilishi, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimewasilisha serikalini mapendekezo ya kuboresha sheria ya marekebisho ya Sheri ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.

Msemaji wa vyama hivyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa mapendekezo hayo yalikabidhiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

Mbatia, ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, alisema hayo baada ya vyama hivyo kukutana jana katika kikao chake cha tatu tangu wakutane na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, jijini Dar es Salaam, Oktoba 15, mwaka huu.

Kikao hicho cha jana, kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Wengine ni Isack Cheyo (aliyemwakilisha Mwenyekiti wa UDP), Nancy Mrindoko (aliyemwakilisha Mwenyekiti TLP), Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa, ambaye aliviwakilisha vyama visivyokuwa na uwakilishi bungeni.

Mbatia alisema kamati ya serikali na ya vyama vya siasa watakutana na kwamba, wamekubaliana mapendekezo hayo yapelekwe katika Mkutano ujao wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo kwa hati ya dharura.

Mbatia alisema suala hilo litajadiliwa katika mikutano ya wabunge wa vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni. Kwamaelezo zaidi BONYEZA WEB hii Katiba kicheko vyama vyote - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Tusubiri tuone kama kweli yamepokelewa na yamo kwenye rasmu au kama yametupwa nje.
 
Mke au Mme wa Rais hayupo kikatiba, wala sio sehemu ya uongozi wa nchi. Familia na Wadhifa/Cheo vitu viwili tofauti kabisa. Lugha ya taifa ni Kiswahili tu, kiingereza nje

Majimbo ya Uchaguzi wakati wowote hayatazidi 150. Hakuna ubaguzi wa aina yoyote na hata wa kijinsi.
 
Mbunge kikomo 15years/three terms Wizara maximum 15years Kodi ya mshahara isivuke kati 10-15% Mshahara kima cha chini usipungue 30% ya kima cha juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…