Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 4,748
- 7,061
Wakuu, heshima kwenu!
Moja kwa moja kwenye hoja yangu.
Hivi karibuni 'Tume huru ya Taifa ya uchaguzi', ilitangaza kuanza kuandikisha/kuboresha/kurekebisha daftari la kudumu la wapiga kura, kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza na Shinyanga, kuanzia tarehe 21 August, 2024 mpaka tarehe 27 August, 2024. Vyama vyote vyenye usajili, vinatakiwa kuwa na wawakilishi/mawakala kwa kila kituo, kwa ajili ya kushuhudia hao wanaoandikishwa.
Cha kushangaza, kuanzia hiyo tarehe 21 August, 2024,mimi binafsi, nimezungukia vituo vinne vya kuandikishia hapa Shinyanga mjini, ni kituo kimoja tu, ndicho nimewakuta mawakala wawili, ikiwa ni wa CCM na wa CHADEMA.
Hivyo vingine vitatu, vina Wakala mmoja mmoja, ambao ni wa CCM peke yao. Na nikanong'onezwa kuwa, CCM inao Mawakala wengine wapo stand by, ikitokea dharula kwa Wakala wa kituo chochote, anakwenda kuchukua nafasi. Pia, nimeshuhudia, Makada wao, wakiwahamasisha wapenzi wao, kwenda kujiandikisha.
Soma Pia: Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wapiga kura wapya 190,131 wanatarajiwa kuandikishwa Mwanza
Sasa, unajiuliza, hivi, tofauti na CCM, hao wengine, wapo tayari kwa mapambano? Pamoja na kuwa ni vigumu kuzuia kila hujuma, lakini kwa style hii, watapona kweli? Hivi yale aliyo "ropoka" Nape Nnauye, wanafikiri ni utani? Hivi, baada ya Uchaguzi, watakuwa na uhalali wa kulalamikia WAPIGA KURA HEWA, au VITUO HEWA?
Vyama vyote ambavyo ni wapinzani wa CCM, hawawatendei haki wapenzi wao! Wanawachosha, na kuwakatisha tamaa kuwaunga mkono!