Vyanzo vya kutetemeka kwa usukani

Vyanzo vya kutetemeka kwa usukani

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
Vyanzo vya kutetemeka kwa usukani

Unakwazika na hali hiyo? Hauko peke yako. Hili ni tatizo kubwa kwa madereva wengi, mara nyingigari hucheza katika mwendo mkubwa na mara zote gari ikianza kutembea. Uzoefu unaonesha kua hili hua ni tatizo katika mfumo wa Chasis au tairi na unahitaji uchunguzi wa kina ili kuondosha kabisa tatizo hili.

Vyanzo vya tatizo hili ni kama ifuatavyo:-

1. Magurudumu yaliyopishana/ Misalligned Tires

Ni moja ya sababu za kawaida za kufanya gari yako ivibrate. Dalili ya shida hii ni kutikiswa kwa magurudumu karibu na mwendo wa 50km/h na kuwa mbaya inapofika 60km/h. Lakini, hupungua wakati Unaongeza Mwendo zaidi. Njia bora ya kuepusha ni kuangalia matairi mara kwa mara ili kujua iwapo matairi yako yamefuatana vizuri bila kupishana.

2. Magurudumu yasiyokuwa na usawa/Unbalanced Wheels

Matairi yasiyo na usawa, yaliyoharibiwa, na yenye ubora duni yanaweza kusababisha kukosekana kwa uimara barabarani. Jambo hili linapotokea, husababisha kutetemeka sana kwa usukani na wakati mwingine gari nzima. Kupuuza hali hii kunaweza kusababisha uharibifu kwenye mfumo wa usukani, kuharibu shack ups na kula tairi.

3. Tatizo kwenye Mfumo wa Shock Ups

Iwapo kuna jambo halipo sawa kwenye shock ups na mfumo wake huweza kusababisha mtetemo katika gari yako. Mara nyingi hali hii hujitokeza kama sehemu ya kukupatia tahadhari ya mambo ambayo huenda yakawa ni chanzo, kwa mfano, kuisha kwa shock ups zako na kutokaza vizuri kwa nati zinazoshikamana na shock ups zako.

4. Matatizo ya Brake

Inapotokea mtetemo ukajitokeza wakati unapopunguza mwendo mara nyingi shida hua ni kwenye mfumo wa brake hivyo zinahitaji kuangaliwa kwa ukaribu. Utakagua Disc, Kukazwa vizuri kwa mikono inayoshikilia break pads na zaidi utakagua Pads zako iwapo zimemalizika.

5. Kuharibika kwa mikono inayoshikilia injini (Engine Mounting)

Mara nyingi hii huweza kusababisha mtetemo wa gari zima hata kama imepaki bila kutembea na mtetemo huo huanzia mbele kwenye injini na huweza kua mkubwa zaidi gari inapoanza kutembea na kufika 30km/h. Ni muhimu kuangalia injini mounting na kubadirisha iwapo utakuta raba zake zimekwisha au ziko loose.
 
Shukran mkuu kwa elimu ya bure kuhusu magari. Nahisi la kwangu litakuwa hili la tano (Engine Mounting)
 
Kuna fundi mchundo aliniulia gari ikakosa radha kabisa. Gari ikikua nzima kbs nikampelekea anichekie brake pads alivofungua na kufunga gari ikawq na mtetemo kama bajaji maanina

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana boss. Unapohitaji fundi vizuri sana ukadodosa historia kwa watu wengine ili kupata picha ya uzoefu wake, ujuzi wake na nidhamu anapokua anatengeneza chombo husika. Wengine hua wanagonga nyundo tuuu na kubomoa vitu vingine
 
Back
Top Bottom