Vyeo kama hivi katika Nchi yetu bado vina ulazima wowote ?

Vyeo kama hivi katika Nchi yetu bado vina ulazima wowote ?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari JF ,Ukiachana na Suala la Udiwani na Ubunge wa viti maalumu bado kuna vyeo vingi sana ambavyo kuna haja ya kuvipitia na kuona kama kuna umuhimu kuendelea kuwepo.

Mfano Wilaya inawakilishwa na watu wafuatao
1. DC
2. DED
3. DAS
4. MP

Lakini pia kuna nafasi za unaibu waziri ,mi nadhani waziri na Katibu wanatosha .

Hivi hakuna namna ya kupunguza watu kwa kuongeza majukumu katika nafasi nyingine ? Itasaidia kupunguza Matumizi .
 
Hii nchi kuendelea itakua ngumu sana tumejaza ma vyeo mengi yanayotumia hela nyingi za walipa kodi kulipa mishahara na miposho mingi kwa nafasi zisizo kuwa na mana.

Angalia bunge linavyokamua fedha za walipa kodi.

Kwa nchi yetu hii wabunge walipasawa wasizidi 150.


#MaendeleoHayanaChama
 
Habari JF ,Ukiachana na Suala la Udiwani na Ubunge wa viti maalumu bado kuna vyeo vingi sana ambavyo kuna haja ya kuvipitia na kuona kama kuna umuhimu kuendelea kuwepo ...
Hivi vyeo tulirithi toka kwa wakoloni tukavitumia bila kuangalia madhumuni na uhitaji.

Hata hao wateuliwa kama vile hawana "job description" maana kila wakati wanazozana kwa kuingiliana kiutendaji.
 
Hii nchi kuendelea itakua ngumu sana tumejaza ma vyeo mengi yanayotumia hela nyingi za walipa kodi kulipa mishahara na miposho mingi kwa nafasi zisizo kuwa na mana...
Mbaya zaidi mishahara mikubwa mno
 
Habari JF ,Ukiachana na Suala la Udiwani na Ubunge wa viti maalumu bado kuna vyeo vingi sana ambavyo kuna haja ya kuvipitia na kuona kama kuna umuhimu kuendelea kuwepo.

Mfano Wilaya inawakilishwa na watu wafuatao
1. DC
2. DED
3. DAS
4. MP

Hivi hakuna namna ya kupunguza watu kwa kuongeza majukumu katika nafasi nyingine ?
DED ni muhimu sn lakini vingine havina maana yoyote zaidi ya ulaji
 
Ata mawaziri na ma naibu wake hawatakiwi kuwapo. Katibu mkuu na katibu mkuu wa kila wizara wanatosha.

Wabunge wabaki na kazi ya kuwakilisha wananchi na kukosoa na kusimamia matumizi ya serikali.

Swala la hotuba na bajeti litakua linasomwa na makatibu kwa kila wizara. Wabunge wanabaki kuchambua na kuamua vya kupitisha. Hii ya kua mbunge na waziri inatengeneza loop fulani ya kupendeleana na wizi pasipo kuwajibishwa.
 
Back
Top Bottom