1. Akh (أَخ) ni ndugu kwa Kiswahili, hivyo kila muislamu ni Akh, akiwa wa kike ukht (أُخْت) Dada. Ilitumika zaidi kwa wafuasi wa Muslim Brotherhood, wengine wanaiga.
2. Sheikh (شَيْخ) literally means Mzee. [ii] Mtu aliewahi kuwa au aliepo kwenye ndoa. Akiwa wa kike Shaikha (شَيْخَة). Si vyeo vya kidini.
3. Ustadh (أُسْتَاذ) ni Profesa. Au [ii] Mwalimu. Maana zote hazihusiki na dini ya Kiislamu. Ni lugha tu.
4. Kadhi (قَاض) Jaji. Anaweza akawa Kadhi wa mahkama ya Kiislamu au conventional. Ili awe Kadhi, ni lazima awe na mamlaka ya kutumia nguvu kama alivyo jaji. Anapotoa hukumu ni lazima wahusika wafuate. Mfano Zanzibar wana makadhi wa wilaya, mkoa na Kadhi Mkuu, Kenya wanamwita Chief Kadhi.
5. Mufti (مُفْتِي) Mtu anaejibu masuala ya dini, anaweza kuwa mufti wa dhehebu maalum au mufti wa jumla. Sio lazima achaguliwe na serikali au awe na mamlaka, kauli yake si lazima kufuatwa, inakua ni legal view. Mfano waendesha vipindi vya "uliza ujibiwe" katika vituo redio na televisheni vya Kiislamu, au Mufti Mkuu wa nchi kama Mufti Menk wa Zimbabwe.
6. 'Aalim (عَالِم) ni graduate. Haijalishi dini. 'Ulamaa (عُلَمَاء) laterally ni graduates, just plural. [ii] Scientist. Pia haina mafungamano na dini.
Mfano Baraza la Ulamaa Tanzania, inamaanisha wao minimum qulification kwa memba wao ni a bachelor degree.
7. Imamu (إِمَام) Kiongozi. Akiwa Imamu wa msikiti ni kiongozi anaeongoza swala. Anapatikana kwa kuchaguliwa na waumini wenyewe, vigezo ni elimu ya Qur'an wakiwa sawa anaejua zaidi Sunnah, wakiwa sawa anatangulizwa mwenye umri mkubwa... na vigezo vyengine vinafuata ikiwa watakua wanalingana.