Vyeo ndiyo sababu ya UVCCM kutotaka Katiba mpya

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
UVCCM wanajua kabisa kua katiba mpya hasa mchakato ulioanzishwa na tume ya Jaji Warioba na ile Pendekezwa hautambui kabisa nafasi za Wakuu wa Wilaya na Mikoa kwa sababu ni Makada wa Chama tawala na pia ni mifumo ya enzi za Nyerere ambako kulikosa na CHAMA NA SERIKALI, wakati huo ilikua ngumu kutenganisha kiongozi wa serikali na chama.

Changamoto nyingi iliyofanywa vyeo vya DC na RC kukataliwa kwenye mchakato wa katiba mpya ni kuwateua wanajeshi toka vyombo na ulinzi na usalama kisha kuwapa vyeo vya kisiasa wanakua Wajumbe wa kamati za siasa za CCM au Chama tawala, maana yake utawalazimisha wavur sare za jeshi wavae mavazi ya kijani na kuwapa kadi za chama, Wengine bado ni vijana umri wao uko 30s-40s, badae mkataba ukiisha wanarudi kazini kuendelea na jeshi, hii hatari sana ushawaonyesha siasa wanajeshi unafikiri siku za usoni itakuwaje?

Bado kama hawa maDC na na RC watabaki basi wasiwe wanachama wa chama chochote wabaki kama watumishi wengine tu.

Sasa nirudi kwenye point tangu ya msingi, Vijana wengi wa UVCCM hawataki kabisa kusikia kitu kinaitwa KATIBA MPYA kwa sababu watakosa ulaji.Wapo tayari kulala nje hata kuumiza watu ili mchakato huu usifanikowe. Kwa ajili ya haraka haraka wanapambania ulaji wao kwa Gharama zozote zile. Wanamsemea Rais wa JMT kua katiba si kipaumbele cha serikali ya CCM wakati ipo kwenye Ilani ya chama. Hawa vijana ni wa kupuuzwa kwa maslahi ya taifa.
 
Sasa wajiandae kisaikolojia,wasije wakachizi, kwani Mama hajawahi kuwaangusha wanae. Kuwa dokeza tu, sababu ya mabadiliko haya makubwa ni kuelekea katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Moja ya kundi la vijana hopeless ni hili la Uvccm. Ukiwalinganisha na Bavicha, ni mbingu na ardhi.
 
You join political party which serves your interest, then you pray that your interests rimes national interests.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…